Rais wa TPN, Phares magesa (mwenye suti) |
RAIS wa Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN) na Mlezi wa kituo cha kulelea yatima cha New Hope Family Group kilichopo Kigamboni, Phares Magesa ameahidi kuendelea kuwalipia ada za shule watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanaolelewa na kituo hicho.
Magesa alitoa ahadi hiyo mwishoni mwa wiki alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambao ni Wanachama wa Jumuiya ya Umoja wamataifa (YUNA MNMA) mahafali yaliyofanyika kituo hapo, jijini Dar es Salaam.
Alisema amekuwa akisaidia watoto wa kituo hicho kwa muda mrefu hivyo alidaia aendelea ila aliwataka watoto hao kuongeza juhudi katika masomo ili wasirudishe nyuma juhudi zake za kuwasaidia.
Magesa aliwataka watoto hao kuwa watulivu na kuongeza juhudi ili siku moja wafikie walipofikia wenzao waliowatembelea waliokuwa wakihitimu elimu ya juu akidai ndio njia sahihi ya kujikwamua kimaisha.
“Naahidi kuendelea kuwasaidia kwani ni wajibu wangu kama mwananchi ila naomba watu wengine wenye uwezo kujitokeza kama mlivyoamua leo kufanya sherehe yenu kwa kula na watoto hao kwani wanahitaji jamii tofauti nao ili kupunguza msongo wa mawazo”, alisema.
Magesa. alitumia pia alitumia nafasi hiyo kuwaasa wanafunzi wanaomaliza chuo cha Mwalimu Nyerere kuwa waadilifu na wenye maadili pindi watakapopata fursa ya kupaja ajira kokote.
Alisema kumekuwa na tabii ya vijana kukosa uadilifu kwa siku za karibu jambo ambalo linashusha heshima ya vijana ambao wamekuwa wakimaliza masomo katika kwa sasa.
Alisema uadilifu ndio jambo muhimu kwa kijana yoyote ambaye anahitaji kusaidia maendeleo ya nchi yake kwani kuenda kinyume kutarudisha maendeleo na kuathiri jamii moja kwa moja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa tawi la (YUNA MNMA) Fredirick Semainda ambaye ameingia madarakani hivi karibuni alisema wao kama vijana waliamua kufanya sherehe ya kuwaaga kaka na dada zao kwa kutembelea kituo hicho ili waweze kutoa mchango wao kwa watoto hao.
Alisema wao katika mikakati yao ya mwaka wamejipangia kufanya shughuli mbalimbali za kijamii hivyo hii ya kutembelea kituo hicho ni moja ya utekelezaji wa mipango yao.
Semainda alisema katika mahafali hayo ya pili tangu kuanzishwa kwa YUNA MNMA wahitimu 52 wametunikiwa vyeti jambo ambalo wanaliona kuwa ni la mafanikio makubwa.
Mwenyekiti huyo alisema wataendelea kufanya shughuli za kijamii kama hiyo waliofanya mwishoni mwa wiki ambapo walishiriki kuandaa chakula cha mchana na watoto hao na kula nao pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo mchele kilo 40, mafuta, sabuni, madaftari, kalamu na nguo.
Aidha alisema katika sherehe hiyo wanafunzi wanachama wa YUNA MNMA walichangisha shilingi 43,000 kwa ajili ya kuwapatia madawa watoto ambao wanaishi katika kituo hicho.
No comments:
Post a Comment