BAADA ya kuwa katika hali mbaya, hatimaye M To The P amezinduka na kuanza kuuliza kuhusiana na rafiki yake Mangwea
M To The P alipelekwa kwenye wodi ya wagonjwa wa
kawaida leo mchana.
“Kweli anaendelea vizuri sana, sasa amepelekwa
kwenye wodi ya wagonjwa wa kawaida,” alisema Ruta Bushoke, msanii wa muziki wa
kizazi kipya anayeishi nchini humo.
Lakini baadaye Mtanzania mwingine anayeishi
nchini humo alisema M To The P amezinduka.
“Jamaa anauliza Ngwea yuko wapi, sasa
tunashindwa hata kumjibu. Lakini kuna wengine wamemuambia kwamba atakuja hivi
karibuni. Ametoka kidogo,” alisema.
Mangwea na M To The P walikutwa na mkasa ambao
ulipelekea Ngwea kuaga dunia nay eye kubaki akiwa katika hali mbaya.
No comments:
Post a Comment