STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, March 1, 2013

Hammer Q, Salha Abdallah kuoana mchana huu Vikindu

Hammer Q
Salha Abdallah



WAIMBAJI nyota wa muziki wa taarab nchini, Hussein Mohammed 'Hammer Q' na Salha Abdallah wanatarajia kufunga ndoa mchana huu huko Vikindu, mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa wanandoa hao watarajiwa ambao walikuwa kwenye uhusiano wa siri kwa muda mrefu, ndoa hiyo itafungwa mara baada ya swala ya Ijumaa kabla ya wanafamilia kujumuikla pamoja kufurahia harusi hiyo.
Hammer Q, aliyetua katika kundi la Five Star alisema tukio hilo la kumuoa Salha aliyepo kundi la Dar Modern ni furaha aliyokuwa akiisubiri kiwa muda mrefu baada ya ndoa yake ya awali kuishia njiani.
"Aisee kaka nilikuwa nakutaarifu kwamba kesho (leo) baada ya swala ya Ijumaa nitakuwa natekeleza ibada ya ndoa kwa kuoana na Salha Abdallah, " alisema Hammer.
Naye Salha mmoja waimbaji wanaoinukia katika miondoko hiyo kupitia kutamba na vibao matata kikiwemo alichokitunga mwenyewe na kubeba jina la albamu mmoja wapo kati ya tatu za kundi lake zilizozinduliwa mwaka jana za Nauvua Ushoga, alisema anashukuru Mungu kumwezesha kupata mume ambaye ni msanii mwenzake.
MICHARAZO inawatakia kila la heri wanandoa hao watarajiwa ikiwakumbusha juu ya umuhimu wa kuishi kwa wema, upendo, amani na furaha wakikumbuka pia kuwa japo talaka ni halali, lakini ni jambo ambalo Allah Subhanna wataala analolichukia...!

No comments:

Post a Comment