STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 9, 2013

Simba kumuadhibu Gaucho, kisa...!

Gaucho alipokuwa akijifua na Simba hivi karibuni kabla ya kushushwa kikosi cha pili
UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba imesema inasubiri kupata ripoti toka benchi la ufundi juu ya kiungo wao nyota,m Abdulhalim Humud 'Gaucho' ambaye ametowekwa katika klabu hiyo tangu alipotakiwa kujiunga na kikosi cha pili cha timu mara walipoumana na watani zao Yanga, Oktoba 20.
Gaucho aliamriwa na makocha wa Simba yeye na kinda, Haruna Chanongo kushuka kikosi cha pili baada ya kuvurunda katika mabao lao la Yanga kutoka sare ya 3-3, lakini inaelezwa hajaonekana kwenye mazoezi ya kikosi hicho na uongozi unasema unasubiri taarifa ya benchi lao ili kuona hatua gani wamchukulie.
Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema leo kuwa, kama ni kweli mchezaji huyo alishindwa kutekeleza agizo la makocha watamchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu walizojiwekea.
Gaucho alidaiwa kucheza chini ya kiwango yeye na Chanongo na kusababisha Yanga kuongoza mabao 3-0 hadi wakati wa mapumziko kabla ya kutolewa na nafasi zao kuchukuliwa na Said Ndemla na William Lucian 'Gallas' na kufanikiwa kurejeshwa kwa mabao hayo na kuisha kwa 3-3.

No comments:

Post a Comment