STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 9, 2013

Tamasha kubwa la European Film kuanza Nov 22

Inline image 2
TAMASHA kubwa la filamu ambalo ufanyika kila mwaka la European Film Festival (EFF2013) lipo tayari kwa mwaka huu na litaanza rasmi tarehe 22 November 2013 kwa kuonyeshwa filamu mbalimbali katika vituo vilivyopangwa ambazo ni Alliance Francaise, Mlimani City Century Cinemax, Goethe-Institut na Nafasi ArtSpace filamu zitaonyeshwa kwa siku tatu tarehe 22, 23 na 24 November 2013.
Tamasha la hili limekusudia kuinua tasnia ya filamu ya Tanzania katika kujifunza utamaduni kutoka Ulaya katika njia ya filamu katika kuimalisha na kukuza utamaduni wan chi husika hivyo ni njia nzuri kwa watengeneza filamu wa Swahiliwood kushiriki katika kujifunza zaidi utengenezaji bora wa filamu.
Inline image 1
RATIBA KAMILI YA TAMASHA HILO
Filamu nzuri na za kusismua kama vile Limbo, Kings, Tea or Electricity, The Great bear na nyinginezo zitaonyeshwa katika kujenga na kutoa nguvu sambamba na elimu burudani kutoka katika filamu husika, ni tamasha muhimu sana kushiriki kujionea tasnia kutoka Ulaya ilivyopiga hatua, KINGILIO NI BURE unaweza kutembelea  www.trinitypromotionstz.blogspot.com kwa habari zaidi.

No comments:

Post a Comment