STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 28, 2015

Ngoma ya Stand, Kagera yalala, Coastal yashinda

http://api.ning.com/files/cPakA0chAEyfyqjZRP3k2djpZ9GyxNW23W69D7FY4fYhsuNz2vmH6gr7yEITcci18IdnTvIgOej4xydmYu8LtJiXW0uQDhCL/16.jpg
Kagera Sugar watakaomaliza dakika 16 na Stand kesho asubuhi
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/HMB_8262.jpg
Stand wanaoongoza bao 1-0 mpaka sasa kabla ya kumalizia dakika 16 kesho
PAMBANO la timu za Stand United na Kagera Sugar linatarajiwa kumaliziwa kesho asubuhi huku wenyeji Stand wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Dakika 16 zilizosalia baada ya pambano hilo kuvunjika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kwenye dimba la Kambarage zitamalizwa saa 3 asubuhi ya kesho, ikiwa ni mara ya pili kwa pambano la ligi hiyo kuchezwa kwa siku mbili mfululizo.
Pambano la kwanza lilikuwa kati ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting lililoisha kwa sare ya 1-1, kila timu ikipata bao katika vipindi viwili, Mtibwa wakitunguliwa dakika 45 za kwanza na waliporudiana walirudisha bao kabla ya kurudiwa tena kwa pambano la Mtibwa na Kagera na matokeo kuisha kwa sare.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo leo, Mbeya City ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting, huku Coastal ikiwa  na kocha mpya, Jamhuri Kihwelu 'Julio' waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo JKT na kuendeleza ubabe kwa wapinzani wao hao.
Bao la Coastal liliwekwa kimiani na Lutimba Yayo na kuleta furaha kwa mashabiki wa Wagosi wa Kaya ambao kitambo walikuwa hawajaonja ushindi wowote.
Katika mchezo wa Mbeya City na Ruvu Shooting wenyeji wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha aibu cha mabao 3-1 toka kwa Yanga walirejesha bao dakika ya 75 kupitia Themi Felix baada ya wageni kutangulia kwa bao la mapema la Yahya Tumbo.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumatano kwa pambano kati ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment