STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 21, 2014

Babi waanza msimu kwa kipigo Malaysia

Babi (kushoto mbele) akiwa na kikosi cha timu yake ya UiTM iliyolala nyumbani mabao 3-2

KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim Babi ameanza vibaya mechi ya kwanza ya mashindano akiwa n klabu yake mpya ya UiTM ya Malaysia baada ya leo kudunguliwa mabao 3-2 katika pambano la Kombe la FA.

Akizungumza muda mfupi uliopita na MICHARAZO, Babi alisema timu yake imelowa nyumbani dhidi ya PBDKT T-Team katika mchezo uliochezwa uwanja wa nyumbani wao wa Mini UiTM, mjini Shah Alam.

Babi alisema pambano hilo lilikuwa kali na lenye ushindani na mwishowe PBDKT T-Team, walibuka na ushindi huku yeye mwenyewe akishindwa kutupia bao lolote.

Ijumaa Babi anatarajiwa kuingoza timu yake kushuka dimba ikiwa ugenini dhidi ya Kuala Lumpur SPA katika mechi ya Ligi Kuu ya Malaysia itakayochezwa kwenye uwanja wa Hang Jebat mjini Melaka.

Baada ya mechi hiyo UiTM itarejea nyumbani tena siku ya Jumatatu kuikaribisha Johor katika pambano jingine  la ligi hiyo.

Katika msimu uliopita timu hiyo anayoichezea Babi ilikamata nafasi ya tisa kati ya timu 12.

No comments:

Post a Comment