Baadhji ya washiriki wa filamu hiyo ya TMT Movie |
Kwa mujibu wa mratibu wa filamu hiyo, Staford Kihore, filamu hiyo imeanza kurekodiwa ikiwa ni moja ya malengo ya Proin Promotion iliyoendesha shindano la TMT, kuwajenga wasanii wa filamu na kuwapa uwezo wa kuigiza na kufanya kazi kimataifa.
Kihore alisema kuwa wanataka kuthibitishia umma kwamba TMT haikuwa kazi bure bali kuwafanya wenye vipaji vya fani hiyo 'kutusua' ili wafike mbali ndani na nje ya nchi.
“Tasnia ipo na inafanya vizuri lakini inahitaji uthubutu kwa kati ya wanaotengeneza sinema wawe tayari kufanya kitu kizuri kinachoweza kuvuka mipaka ndio tunachokifanya sasa baada ya kuwatengeneza kitaaluma wanafanya kazi,”anasema Staford.
Wasanii wa TMT wamefundishwa na kuiva katika fani ya uigizaji na moja ya alama yao wanayojivunia ni pale ambapo wamepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kupitia filamu ya TMT Movie na kuonyesha kile wanachoongea kwa watazamaji na wapenzi wa filamu Swahilihood.
Filamu kubwa ya TMT Movie inatarajiwa kuonyeshwa katika majumba ya Sinema Afrika Mashariki na Ulaya pia sinema inaongozwa na Muongozaji mahiri wa filamu Karabani na imeandikwa na Novatus Mgulusi ‘Ras Nova’ zaidi ya wasanii 200 kushiriki katika filamu hiyo.
Mhusika mkuu wa filamu hiyo ni Milionea kutoka Mtwara kwa maana mshindi wa shindano la TMT, Mwanaafa Mwizango na nyota wote wa TMT, huku wasanii nyota kibao kutoka tasnia ya filamu Bongo wakipatia nafasi za ushiriki wa filamu hiyo inayojenga ajira kwa jamii nzima.
No comments:
Post a Comment