STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 27, 2014

Suarez aitwa 'Stars' ya Uruguay, akitwa Bonge Hispania

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/08/18/1408396240290_wps_5_Barcelona_s_Luis_Suarez_f.jpgWAKATI akitajwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uruguay, Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Luis Suarez amejikuta akibatizwa jina la Bonge, jina ambalo hakuwahi kuitwa hata alipokuwa Liverpool.
Televisheni ya jijini Madrid imemtaja mshambuliaji kuwa ni mwenye uzito kupindukia na kulalamikiwa kuwa anaonekana ni kama mchezaji mstaafu katika taarifa iliyorushwa mchana wa alhamisi siku ambayo Suarez alifunga magoli mawili katika mchezo wa kirafiki akiichezea Barcelona B dhidi ya kikosi cha Indonesian U19.
Ikiwa imesalia mwezi mmoja kabla ya mchezo wa watani wa jadi Clasico katika msimu huu mchezo ambao utakuwa unaashiria kumalizika kwa adhabu ya mshambuliaji huyo kufuatia kumng'ata mlinzi wa timu ya taifa ya Italia mambo yanaonekana kumuendelea kombo nchini Hispania.
Bosi wa Barcelona Luis Enrique amejibu lawama hizo katika mkutano wake na waandishi wa habari akionekana kushangazwa na tuhuma hizo kwa Suarez.
Katika hatua nyingine mshambuliaji huyo amejumuishwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya hapa Uruguay kwa ajili ya mechi za kirafiki za mwezi ujao dhidi ya Saudi Arabia na Oman, shiriksiho la soka (AUF) limesema juzi.
Mshambuliaji mwenye matata wa Barcelona huyo amefungiwa kucheza kwa miezi minne, pamoja na mechi tisa za mashindano za timu ya taifa, baada ya kituko chake cha kumng'ata beki wa Italia Giorgio Chiellini kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Anaweza kucheza kwenye mechi za kirafiki, hata hivyo, baada ya Mahakama ya Michezo (CAS) kuondoa kipengele ambacho kilimfungia kujihusisha na "jambo lolote la kisoka" katika kifungo chake cha miezi minne.
Baada ya kuachwa kwenye kikosi cha mechi za kirafiki za mwezi huu dhidi ya Japani na Korea Kusini, Suarez ameitwa na kocha Oscar Tabarez katika kikosi cha wachezaji 29 kwa ajili ya mechi hizo za ugenini Saudi Arabia Oktoba 10 na Oman siku tatu baadaye.

No comments:

Post a Comment