Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk Hosea |
Na Kipimo Abdallah
KUTOKUWEPO kwa uwazi, uadilifu na uwajibikaji katika mikataba mbalimbali ambayo serikali inaingia na wawakezaji kutoka nje ni moja ya sababu ya kuongezeka kwa rushwa kwa baadhi ya watumishi wa umma na wawekezaji.
Hayo yamebainishwa na Mwahadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi Profesa Humphrey Moshi wakati akizungumza na mwandishi habari hii kwenye kongamano ambalo linaratibiwa na taasisi ya Jukwaa la Sera (Policy Forum).
Alisema kukosekana kwa uwazi katika mikataba mbalimbali ni moja ya sababu ambayo imekuwa ichangia rushwa kwenye michakato na makubaliano mengi ambayo yanahusisha serikali na wawakezaji.
Profesa Mushi alisema Serikali imekuwa inapata kigugumizi katika kuweka wazi baadhi ya mikataba kwa kile kinachodaiwa kuwa ni siri baina ya mwekezaji na serikali jambo ambalo halina ukweli tofauti na rushwa.
“Mimi nimekuwa nikifanya tafiti mbalimbali hasa za mausuala ya kukua kwa uchumi ni wazi kuwa zipo fedha nyingi ambazo zinapotea ambapo mwanzo wake unaanzia kwenye uingia ji wa mikataba hadi katika utekelezaji ambazo zinaelekezwa katika rushwa”, alisema Mushi.
Mwahadhiri huyo wa UDSM alisema kuonyesha kuwa serikali haina dhamira ya kuondoa hiyo changamoto imekuwa ikiwaruhusu wawekezaji hao kutoweka hata akaunti zao wazi kama ilivyo kwa nchi zingine duniani.
Profesa Mushi ambaye pia aliwahi kuwa mshauri wa masauala ya uchimi wa Rais wa Zanzibar Abeid Aman Karume pamoja na Ofisi ya Hazina ya Tanzania alisema iwapo Tanzania itajikita katika uwazi, uwajibikaji na uadilifu maendeleo yatapatikana kwa haraka.
Mchumi huyo mwandamizi alisema ni dhahiri kuwa kumekuwepo kwa ukiukwaji mkubwa katika maamuzi hivyo ni vema kujiangalia upya kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya kwa maslahi ya Taifa.
Alisema Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa fursa mbalimbali ila kukosekana kwa uadilifu na uwazi kwa baadhi ya watendaji rasilmali hizo zipo hatarini kupotea.
No comments:
Post a Comment