|
Simba itavuna nini kwa Polisi Moro leo ikiwa na mapengo ya nyota wake |
|
Mbeya City kubanana na Coastal |
|
Mtibwa Sugar itavuna nini kwa Ndanda leo Jamhuri! |
|
Ndanda kuendeleza undava hata kwa Mtibwa Sugar? |
|
Mabingwa watetezi Azam watakaovaana na Ruvu Shooting |
|
Prisons-Mbeya kuendeleza ubabe wa Yanga |
|
Simba itawamudu maafande wa Polisi Moro? |
|
JKT Ruvu nao kibarua chao kipo kesho kwa Kagera Sugar |
|
Yanga wenyewe kazi yao ni kesho kwa Prisons |
KLABU ya Simba ikiwa bila ya nyota wake wanne, Paul Kiongera, Haruna Chanongo, Issa Rashid 'Baba Ubaya' na kipa Ivo Mapunda inatarajiwa kushuka dimba la Taifa jioni ya leo kupepetana na Polisi Morogoro, huku kocha wake Patrick Phiri akichekelea pambano lao na Yanga kusogezwa mbele wiki moja.
Simba iliyoanza na sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union wiki iliyopita wakati wakiwa mbele kwa mabao 2-0 watawakosa wachezaji hao muhimu katika kikosi cha kwanza kutokana na kuwa majeruhi, hata hivyo kocha Phiri ametamba wachezaji waliosalia kikosini wapo tayari kuisambaratisha Polisi waliorejea ligi kuu tena.
Polisi inayonolewa na nyota wa zamani wa Yanga, Pan Afrika na Taifa Stars, Mohammed Rishard Adolph, ilikaribishwa ligi hiyo kwa kipigo cha mabao 3-1 na Azam wiki iliyopita na leo itakuwa ikitaka kurekebisha makosa, licha ya ukweli pambano hilo ni gumu kwao.
Phiri alinukuliwa wasingependa kurejea makosa ya wiki iliyopita kwa kuhakikisha wanapata ushindi leo ili kujiweka pazuri kabla ya mechi yao ya mwisho kuisubiri Yanga ambapo aliongelea kusogezwa mbele kwa pambano hilo la watani kutoka Oktoiba 12 hadi Oktoba 18 ni faraja na nafuu kubwa kwao.
Pambano la watani limesogezwa mbele kwa wiki moja toka ratioba ya awali ili kupisha mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya taifa, Taifa Stars dhidi ya Benin.
Ukionoa pambano la Simba na Polisi ratiba ya ligi hiyo inaonyesha kuwa, Coastal Union baada ya kuidindia Simba itasafiri hadi mjini Mbeya kupepetana na wenyeji wao Mbeya City, huku Azam itaialika Ruvu Shooting uwanja wa Chamazi, wakati Ndanda Fc itakuwa wageni wa Mtibwa Sugar mjini Morogoro.
Mechi nyingine ni Mgambo JKT baada ya kuizabua Kagera Sugar itakuwa tena nyumbani kuwakaribisha Stand United iliyoanza ligi hiyo kwa kichapo cha amabo 4-0.
Kipute cha pili hiyo kitaendelea tena kesho kwa mechi mbili zitakazochezwa jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa Taifa, Yanga iliyoanza kwa 'mkosi' wa kubamizwa mabao 2-0 na Mtibwa mjini Morogoro itaialika Prisons-Mbeya na JKT Ruvu ya Fred Felix Minziro itaikaribisha Kagera Sugar uwanja wa Chamazi.
No comments:
Post a Comment