STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, December 6, 2013

Samatta akwama tuzo za CAF, Yaya Toure, Tresor Mputu wapeta

Mbwana Samatta akikimbiza mtu uwanjani akiitumikia timu ya taifa
SHIRIKISHO la Soka Afrika limetoa orodha ya wachezaji 10 wa mwisho wa kuwania tuzo kuu ya Mwanasoka Bora Afrika na nyingine ya wachezaji watano wa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika kwa wanaocheza Afrika pekee, huku jina la Mfungaji Bora wa Kombe la Shirikisho, Mbwana Samatta likiwa halipo.
Mbwana anayeichezea TP Mazembe ya DR Congo na ambaye kwa sasa yupo Kenya na kikosi cha timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars alikuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika. 
Hata jivyo CAF imemchuja katika orodha ya mwisho iliyotangazwa ambapo orodha kamili ni kama ifuatavyo kwa wachezaji wanaowania tuzo kuu ni; Yaya Toure Ivory Coast na Manchester City.
Mshindi huyo wa tuzo ya BBC-2013, anashindana na Ahmed Musa CSKA Moscow na Nigeria, Asamoah Gyan na Ghana na Al Ain, Didier Drogba wa Ivory Coast na Galatasaray, Emmanuel Emenike wa Nigeria Fenerbahce, John Obi Mikel wa Nigeria na Chelsea, Jonathan Pitroipa wa Burkina Faso na Stade Rennes, Mohamed Aboutreika wa Misri na Ahly, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund, Vincent Enyeama wa Nigeria na Lille.
Kwa tuzo ya wachezaji wanaocheza Afrika, watano wanaochuana katika hatua ya mwisho ni Ahmed Fathy, Mohamed Aboutreika wote wa Misri na Al Ahly, Rainford Kalaba wa Zambia na Tresor Mputu wa DRC wanaoichezea TP Mazembe ya DRC na Sunday Mba wa Nigeria na Warri Wolves.
Mshindi atatangazwa katika hafla ya utoaji tuzo hizo Alhamisi ya Januari 9, mwakani mjini Lagos, Nigeria.

No comments:

Post a Comment