STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, September 2, 2014

WWF yatoa mafunzo kwa watumishi wa Manispaa ya Kinondoni

http://www.tic.co.tz/media/kinondoni.jpgSHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la WWF, limeendesha mafunzo kwa watumishi wa idara mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni , kuhusiana na ueneaji wa hewa ukaa na matumizi sahihi ya nishati jadidifu nchini.
Mafunzo hayo yametolewa na Mratibu kutoka WWF.  Teresia Olemako aliyesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha  watumishi wa umma wanakuwa na ufahamu juu ya kukabiliana na madhara ya hewa ukaa na umuhimu wa kutumia nishati jadilifu.
Alisema mafunzo hayo yanahusu watumishi kutoka mikoa mitatu ambayo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro na Arusha ambao majiji na miji yao imeingia katika shindano la kimataifa la kukabiliana na utunzaji wa mazingira ambalo litafanyika mwakani kwa kushirikisha nchi 18 duniani, Tanzania ikiwa ni mara ya kwanza.
Olemako alisema juhudi za WWF kwa kushirkiana na ICLEI ni kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya matumizi sahihi ya nishati jadilifu kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira ambao unachangia kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi kote duniani.
“WWF tumejipanga kushirikiana na watumishi wa mikoa hiyo niliyoitaja hapo juu kuhakikisha suala la kupunguza hewa ukaa na kuhimiza matumizi ya nishati jadilifu ni moja ya majukumu yao ambao watatumia mafunzo hayo kuwapatia wananchi elimu zaidi”, alisema.
Mratibu huyo wa Programu ya Nishati Jadilifu alisema mradi huo utakuwa ukitambaulika kwa kauli mbiu ya (Chakula, Nishati, Taka Ngumu na Maji) kutumika kama njia mbadala ya kukabiliana na uharibifu mazingira katika maeneo husika.
Alisema nishati jadilifu ikitumika ipasavyo itakuza uchumi wanchi pamoja na wananchi kwa ujumla kutokana na ukweli haina madhara na ipo kwa wakati wote hivyo ni vema kila mmoja kuwa balozi mzuri katika kuelimisha jamii.
Akizungumzia juu ya shindano hilo alisema ni vema kwa mikoa husika kufanya kila liwezekano ili kuweza kuleta ushindani wa kweli jambo ambalo linaweza kupelekea Tanzania kuibuka na ushindi ambao utakuwa kichochoe cha utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati jadilifu kuongezeka zaidi.
Aidha alisema kutokana na tathmin iliyofanywa na WWF inakadiriwa hadi mwaka 2025 jiji la Dar es salaam litakuwa na wakazi zaidi ya mil. 6.2 huku mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka mara mbili zaidi ya sasa jambo ambalo linahitaji kufanyika maandalizi mapema kabla hali haijawa mbaya.
Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Injinia Mussa Natty, alisema kila idadi ya watu inapoongezeka, miundombinu na mahitaji ya kibinadamu pia huongezeka hivyo kuifanya jamii kuboresha mahitaji muhimu.
Natty alisema kutokana na hali hiyo WWF inapaswa kuongeza juhudi zaidi za kutoa elimu na kusaidia utekelezaji wa miradi ambayo inaweza kuwa na tija kwa Taifa na wananchi wake kwa vizazi vijavyo kwani kutokufanya hivyo kunaweza kuwa sababu ya kuleta mitafaruku mijini.
Mkurugenzi huyo alisema miradi kama hiyo ikiwa endelevu ni wazi kuwa kila mwanajamii atakuwa balozi mzuri wa kuhitaji mbadilo chanya ambao hayatamuathiri yeye na kizazi chache.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza WWF Tanzania kwa kushirikina na WWW Sweden kwa kuja na mradi huu na manispaa yangu ikawa moja wapo naamini tutaufanyia kazi vizuri kwani sisi Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla tumeathirika sana na mabadiliko ya Tania nchi”, alisema.
“Pia kila mmoja wetu ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es salaam, anahitaji kuwajibika katika sehemu yake ili kuhakikisha mahitaji muhimu ya kibinadamu yanapatikana jirani na jamii ili kuiondoa jamii katika hali ya umasikini unaosababisha ukataji na uharibifu wa misitu”, alisema.
Naye Mwanasheria wa Jiji, Philip Mwakyusa aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe alisema jiji limeupokea mradi kwa mikono yote na watatoa ushirikiano kwa WWF ili iweze kutekeleza mradi huo kwa mafanikio makubwa na ya yenye tija kwa jiji.

No comments:

Post a Comment