Suzuki enzi za uhai wake |
Seleman Ramadhan Suzuki Sauti ya Malaika enzi za uhai wake |
Kwa mujibu wa mwanamuziki mwenzake ambaye alikuwa akifuatilia afya yake kipindi akiugua, Ramadhani Mhoza 'Pentagone' ameiambia MICHARAZO, Suzuki amefariki akiwa nyumbani eneo la Magomeni Kagera, jijini Dar es Salaam na huenda akazikwa leo au kesho.
Pentagone aliyefanya kazi na mwanamuziki huyo aliyekuwa na uwezo wa kutunga, kuimba na kurapu katika bendi za Levent Musica 'Wazee wa Kumuvuzisha' na Extra Bongo, alisema Suzuki alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari na alikuwa akitibiwa nyumbani kwa dawa za kienyeji.
"NIlitaka kukutaarifu kubwa swahiba yetu Suzuki hatunaye kwani amefariki usiku wa leo na kwa sasa tunaangalia mipango ya mazishi kwa kuwasiliana na ndugu zake wa karibu," alisema Pentagone ambaye kwa sasa anaiimbia African Stars 'Twnaga Pepeta'.
Enzi za uhai wake, Suzuki anayetokea Kigoma alitamba na bendi za Tabiora Jazz kabla ya kutua Morogoro katika bendi ya Mikumio Sound iliyowahi kutamba na albamu ya Mlinzi wa Godown kabla ya kuitua Levent Musica na baadaye yeye na wanamuziki wenzake watatu, Bob Kissa, Pentagone na Athanas Montanabe walihamia kwa mpigo Extra Bongo na kupakua albamua ya Mjini Mipango.
Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi na MICHARAZO inatoa pole kwa wote walioguswa kwa namna moja au nyingine na msiba huio na kuwaomba kuwa na moyo wa Subira kwa kukumbuka kuwa 'Kila Nafsi Itaonja Mauti' na Sisi ni wa Mola na Kwake Hakika Tutarejea'.
No comments:
Post a Comment