STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 20, 2013

Uchaguzi wa CHANETA ni vita ya Kibira na ShyRose Dodoma

ShyRose Bhanji




Anns Kibira

UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Netiboli Tanzaniua (CHANETA) unafanyika leo mjini Dodoma huku vita vikubwa vikiwa katika nafasi ya Uenyekiti inayowaniwa na wagombea wawili.
Wagombea hao ni Anna Kibira ambaye ni mchezaji wa zamani wa kiongozi wa muda mrefu ambaye mchango wake kwenye mchezo upo wazi, na Mbunge wa Afrika Mashariki na Makamu mwenyekiti wa sasa. Shy-Rose Bhanji, ambaye yupo nje ya nchi kwa sasa.
Kibira alisimamishwa kwa muda usiojulikana na viongozi wenzake waliokuwa wakiongozwa na Mwenyekiti Anna Bayi ambaye hakushiriki uchaguzi wa sasa.
Wagombea hao walipitishwa katika usaili wa wagombea uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma chini ya kamati ya uchaguzi iliyoongozwa na Betty Mkwasa.
Wagombea wengine waliopitishwa katika usaili huo ni wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti: Zainabu Mbiro na Agnes Mangasila, wakati nafasi ya mweka hazina ni Agnes Hatibu.
Akizungumza na gazeti hili, Betty Mkwasa alisema wagombea wote wametimiza vigezo vilivyotakiwa kwenye fomu ya uchaguzi mkuu, jambo ambalo halikuwa kikwazo katika usaili.
Mkwasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma aliwataja wagombea wa nafasi ya ujumbe ambao wamepitishwa kwenye usaili kuwa ni Yasinta Silvester, Mwajuma Kisengo, Mary Protas, Rose Kisiwa, Judit Ilunda, Hilder Mwakatobe, Penina Igwe, Asha Sapi na Fotunata Kabeja.
"Hawa ndio wagombea watakaopigiwa kura katika uchaguzi mkuu," alisema Mkwasa.
Naye kaimu katibu wa CHANETA anayemaliza muda wake Rose Mkisi alisema mikoa iliyowasilisha wajumbe kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi huo ni Dar Es Salaam, Kagera, Pwani, Mbeya,Dodoma, Manyara, Mwanza na Katavi.


No comments:

Post a Comment