![]() |
Chistian Benteke akishangilia bao lake aliyoisaidia Liverpool kushinda usiku wa jana |


Pambano hilo pekee la Ligi Kuu ya England lililochezwa usiku wa jana lilipigwa kwenye Uwanja wa Anfield na iliwachukua wenyeji dakika 27 kuandika bao hilo tamu baada ya Benteke kuunganisha pasi ya nahodha wake, Jordan Henderson.
Ushindi huo umeifanya Liverpool kukwea hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 6 sawa na vinara, Manchester City na Manchester United,huku wageni hao wa EPL wakikamata nafasi ya 19 wakiwa hawana pointi hata moja kama ilivyo kwa Sunderland wanaoburuza mkia.
Kipute hicho cha Ligi ya England kitandelea wikiendi hii na Jumatatu ijayo.
No comments:
Post a Comment