STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 18, 2015

Yanga warudi Dar, wakitamba kuiva tarari kuiua Azam

MABINGWA wa Soka Tanzania Yanga inatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam leo Jumanne ikitokea Mbeya ilipoenda kupiga kambi ya siku kama 10 na kucheza mechi tatu za kirafiki na timu za jijini humo.
Yanga ilianza kuumana na Kimondo Fc na kuishinda kwa mabao 4-1 kabla ya kuicharaza Prisons-Mbeya kwa mabao 2-0 na kumaliza kazi kwa Mbeya City ikiichapa mabao 3-2.
Kikosi hicho kilinatarajiwa kutua leo na kuingia kambini moja kwa moja kusubiri pambano lao dhidi ya Azam ambao walijichimbia Zanzibar na leo nao watarudi jijini Dar es Salaam kusubiri pambano hilo la Ngao ya Jamii liatakalopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.
Kocha wa Yanga Hans Pluijm amenukuliwa kwamba kikosi chake kimeiva na kazi waliyoenda kuifanya Mbeya imemalizika na sasa ni kuonyesha makali yao hasa kuimarika kwa safu yao ya ushambuliaji.
Pluijm anasema washambuliaji wake wameonekana kukamilika kwa michezo hiyo mitatu na ana tumaini kubwa la kuilaza Azam ambayo ina rekodi ya kucheza mechi 11  mfululizo bila kuruhusu nyavu zake kuguswa, kati ya michezo 12 iliyocheza chini ya kocha Stewart Hall.
Mechi pekee iliyoruhusu wavu wao kuguswa kabla ya kukaza buti ni ile ya kirafiki dhidi ya Friends Rangers ambapo walishinda kwa mabao 4-2.
Baada ya hapo imekuwa ikiendelea kugawa dozi, lakini bila kuruhusu bao langoni mwake kuanzia kwenye michuano ya Kombe la Kagame iliyotwaa msimu huu kwa mara ya kwanza na hata mechi nyingine za kirafiki.
Azam licha ya kushiriki mechi za Ngao ya Hisani mara tatu haijawahi kushinda hata mara moja, mwaka 2012 ilipoteza mchezo kwa Simba kwa kupigwa mabao 3-2, kabla ya kulazwa bao 1-0 na Yanga mwaka uliofuata na mwaka jana ilipigwa mabao 3-0.
Redodi za Azam chini ya Hall baada ya kurudishwa kwa mara ya tatu;

Azam 4-2 Friends Rangers (kirafiki-Dar)
Azam 1-0 JKT Ruvu (kirafiki-Dar)
African Sports 0-1 Azam (kirafiki-Tanga)
Coastal Union 0-1 Azam (kirafiki-Tanga)
Azam 1-0 KCCA Uganda (Kagame-Dar)
Azam 2-0 Al Malakia Sudan Kusini (Kagame-Dar)
Azam 0-0 (pen 5-3) Yanga (Kagame-Dar)
Azam 1-0 KCCA-Uganda (Kagame-Dar)
Azam 2-0 Gor Mahia Kenya (Kagame-Dar)
KMKM 0-1 Azam (Kirafiki-Zanzibar)
Mafunzo 0-3 Azam (Kirafiki-Zanzibar)

No comments:

Post a Comment