STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 15, 2015

Azam wazidi kunoa makali Zanzibar

11846696_1009621735744849_7161429854397873130_n
Kikosi cha Azam kilipopelekea Kombe lao la Kagame Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete
BAADA ya kuikong'ota KMKM ya Zanzibar katika pambano lao la kirafiki, mabingwa wa Kombe la Kagame, Azam jioni ya leo inatarajiwa kushuka Uwanja wa Amaan kucheza mchezo wake wa pili visiwani humo wakiwa wamepiga kambi kujiandaa na mchezo wao wa Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga wikiendi ijayo.
Azam chini ya kocha Stewart Hall imejichimbia humo ikiwa na kikosi chake chote isipokuwa Allan Wanga aliyepo Kenya alipoenda kwa matatizo, huku Mganda Brian Majwega akiwa ametemwa rasmi kikosini.
Mabingwa hao wanajaribu kusaka ushindi kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya Ngao ya Hisani kwani tangu mwaka 2012 haijawahi kushinda mbele ya Simba na Yanga waliowatungua mara mbili mfululizo ikiwamo mwaka 2013 walipowafunga bao 1-0 na mwaka jana kuwafumua mabao 3-0.
Azam inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam Jumanne baada ya kuwepo kwa taarifa ya ziara ya TP Mazembe kufutwa rasmi, na kabla ya kutimka visiwani inaelezwa kuwa huenda ikaiita URA ambayo leo inashuka Uwanja wa Taifa kucheza na Simba katika pambano la kirafiki la kimataifa, ili angalau kuwapa makali ya kuikabili Yanga ambayo ina hasira ya kung'olewa kwenye Kombe la Kagame kwa matuta.

No comments:

Post a Comment