STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 15, 2015

Huku Simba, kule Yanga Utamu Ulioje!

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2015/08/KIKOSI.jpg
Kikosi cha timu ya Simba
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgBANjTf-2fkrx3RLm5RPaUrUbyBwYcFEdzPN7vo1to9_q2hUECoRKM5sjZMEd6wKlYjM72Itb9JeMgpbevjrJZAmBeXrbFiVN2ohR7iP20AWcyQ7rwfR__s4p6_Gx2dc7gmy0Ivy3BZ6R/s640/DSC_6726.JPG
Mabingwa wa Tanzania Yanga
WAKATI kocha Dylan Kerr akiwa na mtihani mwingine mgumu wa kutaka kuwathibitishia mashabiki wa Simba kwamba kikosi chake kimeiva wakati jioni ya leo Jumamosi watakabiliana na URA ya Uganda, watani zao Yanga wenyewe wataendeleza libeneke lao jijini Mbeya kesho kuwa kuumana na Mbeya City.
Mechi hizo za kirafiki ni maalum kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu, ambapo Simba yenyewe baada ya kuweka kambi ya mwezi mmoja na ushei katika wilaya ya Lusohoto, Tanga na Zanzibar imerudi jijini Dar es Salaam ikijifua Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini na leo itaumana na URA Uwanja wa Taifa.
Mechi hiyo ni ya sita kwa Kerr tangu apewe jukumu la kuinoa timu hiyo akimpokea Goran Kopunovic, akiwa na rekodi ya kushinda mechi zote, zikiwemo tano na timu za visiwani Zanzibar na moja ya kimataifa walipoumana na SC Villa ya Uganda kwenye tamasha la Simba Day Jumamosi iliyopita.
Simba inatarajiwa kuwatumia nyota wake wale wale iliyowatumia katika mchezo wao na Villa, huku ikiwa imeshamalizana na nyota wao wa kimataifa, Vincent Agban na Justice Majabvi.
Yanga wenyewe ambao wamekimbilia Tukuyu Mbeya baada ya kutolewa Kombe la Kagame, kesho Jumapili itaumana na Mbeya City katika mechi yao ya tatu jijini humo, awali ilianza kwa mkwara kwa kuitandika Kimondo Fc ya Mbozi kwa mabao 4-1 kabla ya bkuizabua Prisons Mbeya kwa mabao 2-0 na baada ya mchezo hio wa kesho itawasubiri Zesco ya Zambia na Bata Bullets ya Malawi kumaliza kazi kabla ya kurudi Dar kuisubiri Azam kwenye pambano la Ngao ya Hisani litakalochezwa Jumamosi ijayo.
Mechi hiyo ya Ngao ya Hisani itakayopigwa Uwanja wa Taifa ni maalum katika kuzindua msimu mpoya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara amabyo itaanza kutimua vumbi lake, Septemba 22.

No comments:

Post a Comment