STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 15, 2015

Mtaipendaje Simba? Baada ya Agban kusaini sasa zamu ya Mzenji

Simba Day
Simba wakishangilia ushidni wa mechi yao na SC Villa ya Uganda siku ya Tamasha la Simba Day
KLABU ya Simba kwa hakika imepania msimu huu, kwani baada ya kumlambisha mkataba wa miaka miwili kiungo wake wa Kizimbabwe, Justice Majabvi, iliona haitoshi, ikamsainisha tena kipa Muivory Coast, Vincent Agban. Sasa kama  ulidhani walishamaliza kazi, umekosea kwa sasa klabu hiyo imemuita jijini kipa wa JKU-Zanzibar, Mohammed Abdulrahman ili kumalizana naye.
Kipa huyu ndiye waliyewahi kumtangaza mapema kwamba imemnasa kisha ikabainika kuwa bado ana mkataba mrefu na klabu yake kama ilivyokuwa pia kwa straika wa Vital'O, Laudit Mavugo.
Baada ya kutafakari kwa kina na hasa kutokana na kipa Ivo Mapunda kuwadengulia tangu wampe Sh. Milioni 10 za kusaini mkataba mpya, Simba ilipiga hesabu kumleta kipa Mbrazili, Ricardo Andrade, lakini ikamshtukia ana umri mkubwa mno, hivyo wakaachana naye.
Ndipo wakaamua kurudi kwa Abdulrahaman ambaye leo hii atatua jijini Dar es Salaam kumalizana na viongozi wa Simba tayari kuidakia timu hiyo katika michuano ya Ligi Kuu msimu wa 2015-2016.
Viongozi wa Simba wamekuwa wasiri katika suala la kipa huyo, lakini MICHARAZO inafahamu kuwa Abdulrahaman jana alikuwa Bububu na leo Jumamosi atapata boti kuitikia wito wa viongozi wa Simba ambao wiki sasa wamekuwa wakifanya mazungumzo naye na klabu yake ya JKU itakayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani,
Simba tayari imeshamshainisha kipa Agban aliyewahi kufanya majaribio timu ya vijana ya Chelsea na kuonekana kijeba na mwezi mmoja uliopita alikuwa akijifua na Azam kusaka nafasi ya kusajiliwa kabla ya kocha Stewart Hall kumpotezea kwa kuamini kazi nzuri ya Aisha Manula na Mwadini Ali.

No comments:

Post a Comment