STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, August 18, 2015

Maxime kutumia kasi ile ile iliyopita kufunika VPL

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/03/Mecky-Mexime1.jpg
KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa ile kasi waliyoanza nayo msimu uliopita ndiyo watakayoitumia msimu ujao kuweza kurejesha heshima ya mabingwa hao wa zamani.
Mtibwa iliianza ligi ya msimu uliopita kwa mkwara ikishinda mfululizo na kuongoza msimamo hadi ligi iliposimama Novemba 9, kisha kwenda kwenye Kombe la Mapinduzi na kufika fainali dhidi ya Simba.
Baada ya kichapo cha Simba cha mikwaju ya penalti, Mtibwa ilirudi katika ligi kuu kichovu na kupoteza mechi mfululizo, kiasi cha kuwa hatarini kushuka daraja kabla ya kuzinduka mwishoni.
Hata hivyo Maxime, alisema kwa namna anavyowaandaa vijana wake ana hakika mambo yatakuwa bambam katika msimu ujao ili kurejesha heshima ya klabu yao.
Maxime anasema ingawa hana maproo waka kufanya usajili mkubwa, lakini kurejesha baadhi ya majembe yake kama Issa Rashid 'Baba Ubaya', Said Bahanuzi na kipa Hussein Sharif 'Casillas' ni vitu vinavyompa jeuri kuamini msimu ujao wapinzani wao lazima wakae.
Mtibwa iliwahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka 1999 na 2000 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutwaa mataji mengi nje ya Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikipokezana miaka nenda rudi.
Pili ilikuwa ni klabu ya kwanza nje ya Dar kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo.

No comments:

Post a Comment