STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 23, 2013

Redock Mauzo wa Extra Bongo kutoka kivyake

Redock Mauzo katika pozi
 MWIMBAJI mahiri wa bendi ya Extra Bongo, Redock Bokasa 'Mauzo', anajiandaa kupakua wimbo mpya uitwao 'Ahadi ya Mapenzi' ikiwa ni maandalizi ya kutoa albamu binafsi.
Akizungumza na MICHARAZO, Redock aliyewahi kung'ara na bendi ya Bambino Sound na TOT-Plus, alisema tayari wimbo huo mpya umekamilisha kurekodiwa na anaufanyia mpango wa kuotoa hadharani ili uanze kusikika hewani.
Redock mwenye asili ya Kongo (DRC) alisema wimbo huo uliopigwa katika miondoko ya rhumba ni wa pili katika maandalizi ya albamu hiyo ijayo, kwani wimbo mwingine uitwao 'Sandra' aliowahi kuutoa akiwa Kongo na kuja kuurudia kwa jina la Zai alipokuwa TOT ni miongoni mwa nyimbo za albamu hiyo.
"Nimekamilisha wimbo wangu mpya uitwao 'Ahadi ya Mapenzi' kwa ajili ya albamu yangu niliyopanga kuitoa baadaye ikiwa na nyimbo nane, mwingine unaitwa Sandra utakuwa miongoni mwao," alisema Redock.
Alisema nyimbo nyingine amekamilisha mashairi yake tu na bado hajaanza kuzifanyia kazi ili kuziingiza studio kuzirekodi kwa sababu ya kutingwa na majukumu yake ndani ya Extra Bongo inayojiandaa na maonyesho ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

No comments:

Post a Comment