STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 23, 2013

Mhe Temba, Cassim wana Monti Kochi

Cassim
Mhe Temba

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Amani Temba 'Mheshimiwa Temba' ameachia wimbo mpya uitwao 'Monti Kochi' alioimba akishirikiana na mkali wa zamani wa Tip Top Connection, Kassim Mganga 'Cassim'.
Meneja wa msanii huyo, Said Fella aliiambia MICHARAZO kuwa, wimbo huo umeanza kusambaza katika vituo vya reido ili kuanza kurushwa hewani.
Alisema wimbo huo umerekodiwa chini ya prodyuza Shedrack Moigi maarufu kama Shedy Clever wa Burn Records, aliyeutengeneza wimbo unaotamba wa mkali Diamond uitwao 'The Number One'.
"Baada ya Chegge kutoka na Chapa Nyingine, membaz mwenzake wa TMK Wanaume, Mheshimiwa Temba ameachia wimbo uitwao 'Monti Kochi' alioimba na Cassim Mganga, utaanza kusikika hewani kwani tumeanza kuusambaza katia vituo vya redio," alisema Fella.
Fella alisema video ya wimbo huo itafuata baadaye, japo alisema kazi hiyo inaweza kufanywa mapema kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.



No comments:

Post a Comment