STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 23, 2013

Inter Milan waikausha AC MIlan Seria A, Muntari akilimwa RC jioni

AC Milan's forward Mario Balotelli kicks the ball during the Italian Serie A football match Inter Milan vs AC Milan at San Siro Stadium in Milan on December 22, 2013
Mario Balotelli akikosa bao la wazi langoni mwa Inter Milan
AC Milan's French defender Kevin Constant fights for the ball with Inter Milan's Argentinian forward Rodrigo Palacio during the Italian Serie A football match on December 22, 2013
Inter Milan's Argentinian forward Rodrigo Palacio celebrates after scoring during the Italian Serie A football match Inter Milan vs AC Milan at San Siro Stadium in Milan on December 22, 2013
'Muuaji; akishangilia bao lake
BAO lililofungwa na Rodrigo Palacio dakika nne kabla ya kumalizika kwa pambano la watani wa jadi wa mji wa Milan, liliisaidia Inter Milan kupata ushindi muhimu dhidi ya mahasimu wao Ac Milan katika mechi ya Ligi Kuu ya Italia, Seria A lililochezwa usiku wa kumakia leo.
Licha ya kipigo hicho pia, Milan ilipata pigo dakika za lala salama wakati kiungo wake, Sulley Muntari alipolimwa kadi nyekundu wakati mchezo ukielekea kumalizika.
Palacio raia wa  Argentina aliifungia Inter bao hilo akimalizia kazi nzuri ya Fredy  Guarin na kuzidi kuicha Milan izidi kuchechemea kwenye ligi hiyo ikishika nafasi ya 13, huku wapinzani wao kwa ushindi huo wamekwea hadi nafasi ya tano ikifikisha pointi 31.
Kipigo hicho kimekuja baada ya Milan kupata sare mfululizo katika mechi zake za hivi karibuni katika ligi na kuliacha benchi la ufundi la mabingwa hao wa zamani wa Ulaya wakiweweseka kujiweka sawa kabla ya kuwakuta yaliyowakuta makocha wa klabu nyingine waliotimuliwa.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Livorno ililala nyumbani kwa mabao 2-1 dhidi ya Udinese, Cagliari ililazlimishwa sare ya 1-1 na Napoli kwa mechi zilizochezwa Jumamosi.
Mechi zilizochezwa jana Bologna ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Genoa, Atlanta ikalala kwa mabao 4-1 nyumbani kwake mbele ya mabingwa watetezi Juventus, huku Hellas Verona ikiishindilia Lazio kwa mabao 4-1.
Nayo Roma iliendeleza mauaji kwa kuilaza Catania kwa mabao 4-0,  Sampodoria na Parma zikitoka sare ya 1-1 na Fiorentina ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Sassuolo na Chievo Verona ikilala ugeninikjwa mabao 4-1 toka kwa Torino.

No comments:

Post a Comment