STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 23, 2013

Chegge Chigunda aweka Chapa Nyingine videoni

Chegge katika pozi
MKALI wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la TMK Wanaume Family, Said Juma 'Chegge Chigunda' ameanza kushuti video ya wimbo wake mpya wa 'Chapa Nyingine' unaoendelea kutamba katika chati za redio.
Meneja wa TMK, Said Fella aliiambia MICHARAZO kuwa, video hiyo imeanza kushutiwa tangu Jumatano chini ya mtaalam Adam Juma wa Visual Lab na inatarajiwa kukamilika siku ya leo.
Fella alisema video hiyo inarekodia kwenye maeneo tofauti ya jiji kwa lengo la kuipa mandhari ya kuvutiwa mara itakapohaririwa itaachiwa pengine wiki ijayo ili mashabiki wapate burudani.
"Tupo mtaani kwa sasa tukirekodi video ya wimbo mpya wa Chegge uitwao Chapa Nyingine na tunatarajia kuanza kusambaza pengine wiki ijayo kama itahaririwa mapema," alisema Fella.
Aidha, Fella anayekimiliki pia kituo cha kuibua na kukuzia vipaji cha Mkubwa na Wanae, alisema kuwa wimbo mpya wa mwanadada Sarah Kais 'Shaa'; wa 'Sifa Ujinga' umekamiliki kwa kurekodiwa 'audio' na video yake, ila wameuweka pembeni kutoa nafasi kwa wimbo wa 'Sugua Gaga' kuendelea kutamba hewani.
"Unajua wimbo wa 'Sugua Gaga' umetoka muda mfupi uliopita na unaendelea kufanya vyema sokoni, hiyo tunahofia kuachia 'Sifa Ujinga' mapema ndiyo maana tumeubana mpaka mapema mwakani," alisema.
Shaa, alitua kwa Mkubwa na Wanae inayomilikiwa kati ya Fella na Babu Tale kwa mkataba wa miezi sita akitokea kwa Master J na 'Sugua Gaga' ndiyo kazi ya kwanzaa kutoa chini ya mabosi wake hao.

No comments:

Post a Comment