STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 23, 2013

Side Boy Mnyamwezi usimdharau Ney wa Mitego

Side Boy katika pozi
BAADA ya ukimya mrefu tangu alipotoa 'Hujafa Hujaumbika', msanii mahiri wa miondoko ya Bongofleva anayejishughulisha na ujasiriamali, Said Salim 'Side Boy Mnyamwezi', ameachia wimbo mpya 'Usimdharau Usiyemjua' .
Wimbo huo mpya ambao umeshaanza kurushwa hewani kupitia mitandao ya kijamii na vituo vya redio umerekodiwa kwenye studio za Pamoja Records na ameuimba akishirikiana na Ney wa Mitego.
Side Boy aliyewahi kutamba na nyimbo kama 'Kua Uone', 'Jifungue Salama' na 'Pongezi wa Kikwete', alisema wimbo huo ni utambulisho wa albamu yake ya tatu anayojiandaa kuitoa mapema mwakani.
Alisema albamu hiyo ijayo inayofuata baada ya zile za 'Kua Uone' na 'Acha Waseme' na ataitoa katika muundo wa CD mbili kwa moja ikijumuisha video na audio, ili kuwapa raha mashabiki wake na wale wa muziki wa ujumla.
"Albamu yangu ijayo ambayo bado sijaipa jina itatoka ikiwa na CD mbili, moja video na nyingine au audio ili mashabiki wasisumbuke," alisema.,
Msanii huyo aliyewahi kufanya kazi pamoja na kundi la TMK Wanaume Family, japo hakuwa 'memba' wa kundi hilo, alisema mashabiki wake wajiandae kupata ladha mpya toka kwake kutokana na albamu hiyo ya tatu anavyoiandaa kwa sasa itakayokuwa na nyimbo nane.

No comments:

Post a Comment