Harry Keane akifunga moja ya mabao yake ya 'Hat Trick' |
Entiene Couples akimiliki mpira |
Wachezaji wa Fiorentina wakishangilia bao lao la dakika ya 38 lililowapa ushindi ugenini |
Samuel Eto'o akijaribia kuipigania Everton mbele ya Lille bila mafanikio timu hizo zilitoka 0-0 |
Spurs ambayo imekuwa ikichechemea kwenye Ligi Kuu ya England, ilipata ushindi huo ikiwa nyumbani kwa mabao yaliyofungwa na Harry Kane aliyefunga 'hat trick' katika dakika ya 13, 75 na 81, wakati Erik Lamela 'Rabona' aliyesajiliwa kwa Pauni Mil. 30 alifunga mengine mawili katika dakika ya 29 na 66.
Wageni walipata bao lao dakika ya 89 kupitia kwa mtokea benchi, Jeronimo Barrales aliyefunga kwa mpira wa adhabu na kufanya Spurs kumaliza mechi hiyo ya kundi C wakiwa wababe kwa mabao 5-1.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo Besiktas iliisasambua Partizan nyumbani kwao kwa mabao 4-0, huku kwenye mechi za makundi mengine Everton ikiwa ugenini ililazimishwa shuluhu na Lille ya Ufaransa.
Matokeo mengine ni kama yafuatavyo;
Metalist 0-1 Legia Warszawa,
Krasnodar 2-4 Wolfsburg
Rijeka 3-1 Feyenoord
Standard Liège 0-0 Sevilla
Lille 0-0 Everton
Slovan Bratislava 0-3 Sparta Praha
Young Boys 2-0 Napoli
AaB 3-0 Dynamo Kyiv
Steaua Bucureşti 2-1 Rio Ave
Dinamo Minsk 0-0 Guingamp
PAOK 0-1 Fiorentina
Trabzonspor 2-0 Lokeren
Villarreal 4-1 Zürich
Borussia M'gla… 5-0 Apollon
Torino 2-0 HJK
Club Brugge 1-1 København
Celtic 2-1 Astra
Salzburg 4-2 Dinamo Zagreb
Estoril 1-2 Dinamo Moskva
PSV 1-1 Panathinaikos
Internazionale 0-0 Saint-Étienne
Dnipro Dniprop… 0-1 Qarabağ
No comments:
Post a Comment