NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema hawazii suala la kushindwa kwake kuvunja rekodi ya mabao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inayoshikiliwa na Raul aliyokuwa na uwezo wa kufanya hivyo wakati walipoiangushia kipigo Liverpool kwa madai kuwa anaweza kuivunja katika mechi nyingine.
Ronaldo alibakisha goli moja kuifikia rekodi ya Raul baada ya kufunga bao lake la 70 katika ushindi wa 3-0 kwenye Uwanja wa Anfield, idadi ambayo inamtangulia Messi kwa bao moja.
Mreno huyo alikuwa na nafasi nyingi za kuweza kuifikia na hata kuipita rekodi hiyo lakini alibaniwa na kipa wa wenyeji, Simon Mignolet.
Lakini hakuwa mnyonge kutokana na jambo hilo hata hivyo, na akaiambia Sky Sports: "Sihofii kuhusu rekodi. Najua nitaipiku tu, kama haijawa leo, basi itakuwa katika mechi nyingine. Messi ameikaribia pia."
Ronaldo ambaye alikuwa hajawahi kufunga goli Anfield tangu alipokuwa akiichezea Manchester United, alisema: "Ilikuwa ni 'spesho', goli langu la kwanza hapa Anfield na najivunia kwa hilo. Tumepata pointi tatu, ilikuwa ni babkubwa."
Mshambuliaji huyo aliye katika kiwango cha juu ambaye sasa amefunga magoli 20 katika mechi 13 za michuano yote msimu huu, alisema inawezekana wao wakawa timu ya kwanza kutetea taji la Klabu Bingwa Ulaya licha ya kwamba haitakuwa rahisi.
Mshambuliaji huyo kesho anatarajiwa kuiongoza timu yake katika pambano la kwanza la El Classico kwa msimu huu dhidi ya Barcelona, ambayo nyopta wake Lionel Messi anatarajiwa kuvunja rekodi ya mabao ya La Liga kama atafanikiwa kufunga katika mchezo huo zaidi ya bao moja.
No comments:
Post a Comment