STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 17, 2013

Uongozi wa Shule awatolea uvivu wazazi, kisa...!


Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Makumbusho
UONGOZI wa Shule ya Msingi Makumbusho umewajia juu wazazi kwa tabia yao waliyonayo ya kushindwa kutoa ushirikiano wa kutosha hasa kwa watoto wao wasiojua kusoma na kuandika na kutishia kuanzia mwakani hawatapokea mtoto yeyote ambaye hajapitia shule ya awali.
Pia uongozi huo umesema kuanzia sasa shule yao itaanza kuwatimua wanafunzi wote watakaokuwa na maendeleo duni darasani ili kuiepushia aibu shule yao.
Mwalimu Mkiuu wa Shule hiyoi,  Mama Lyimo akizungumza na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo katika kikao cha pamoja kilichofanyika jan Ijumaa, alisema uongozi wao wamekuwa na wakati mgumu kwa wazazi wasiopenda kuotoa ushirikiano kwa walimu.
Mwalimu Lyimo alisema walimu wamekuwa wakitaka kuwasaidia baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika, lakini wamekuwa wakikosa ushirikiano kwa wazazi wa watoto hao pale wanapoitwa shuleni kujadiliana nao kitu kinachowakatisha tamaa.
"Wazazi mnatukatisha tamaa katika kuwasaidia watoto wenu kwa kushindwa kutupa ushirikiano pale mtunawapowaita tuje kujadiliana namna ya kuwainua watoto wenu ambao baadhi huwa hawajui kusoma wala kuandika," alisema.
Aliongeza walimu pekee yao hawawezi kuwasaidia watoto wenye matatizo hayo bila kupata ushirikiano kwa wazazi, hivyo akawahimiza baadhi ya wazazi kuwe wepesi kuitikia wito wa walimu wanapoitwa kwa sababu wakati mwingine ni faida kwao na watoto zao.
Alisema kwa idadi kubwa ya wanafunzi ndani ya darasa moja huwa vigumu kwa walimu kufanya kazi yake kwa ufasaha, hivyo kuwaita wazazi kunaweza kurahisisha kuwatatulia matatizo wanafunzi, lakini wazazi wamekuwa wazito kitu kinachowasononesha.
Mwl Lyimo alisema katika kuhakikisha shule yao inaepukana na kuwa na watoto wasiojua kusoma wala kuandika kuanzia mwakani hawatawapokea wanafunzi wa darasa la kwanza wasiopitia elimu ya awali kwa uthibitisho wa vyetu vya kuhitimu shule hizo.
"Hili ndilo tunalohisi ni suluhu ya kwanza ya kuepuka shule yetu kuwa na mambumbumbu, hatutapokea mwanafunzi wa kuanza darasa la kwanza bila kuwa amepitia masomo ya awali ambayo huwarahisisha kujua kusoma na kuandika," alisema.
Nao baadhi ya wazazi walitoa lawama zao kwa walimu ambao wanashindwa kuwafundisha watoto wao vyema darasani na kulazimisha wasome masomo ya ziada (twisheni) na kudai jambo hilo limekuwa likiwaumiza wanafunzi wenye uwezo mdogo wa kifedha.
"Kuwalazimisha watoto wabaki kwa ajili ya twisheni kunapelekea watoto wasio na uwezo wa kulipa masomo hayo kukosa masomo kikamilifu kutokana na ukweli walimu wamekuwa wakifundisha vyema huko kuliko darasani, hii siyo sawa, walimu badilikeni," alisema mmoja wa wazazi waliohudhuria kikao hicho.
Shule hiyo ya Makumbusho imekuwa na desturi ya kuitisha kikao pamoja na wazazi mara kwa mara kwa nia ya kujadili na kutathmini maendeleo ya wanafunzi na shule kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment