STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 24, 2014

Beki Atletico Madrid presha tupu dhidi ya Real Madrid jumapili

https://pbs.twimg.com/profile_images/378800000708295411/f912c666061f41dffd5b2d51ee982b30.jpeg
Filipe Luis wa Atletico Madrid
BEKI wa Atletico Madrid, Filipe Luis amesema akili zao kwa sasa zipo kwenye mechi yao ijayo dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Madrid, Real Madrid.
Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumapili kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Hispania huku zikiwa kwenye mbio za kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Barcelona.
Vijana wa kocha Diego Simeone wataivaa Real wakiwa wanauguza kipigo cha mabao 3-0 walichopewa jana ugenini na Osasuna, ambapo Filipe alisema wasingependa kurudia makosa katika mechi hiyo ya mahasimu wao.
Makosa yaliyofanywa na safu yake ya Atletico yaliifanya wenyeji kupata mabao hayo matatu yaliyoibakisha timu hiyo kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Barcelona wakiachwa pointi tatu nyuma na Real Madrid wanaoongoza msimamo wa ligi.
Beki huyo wa Kibrazil, anafahamu ugumu unaowakabili dhidi ya timu hiyo kwenye kiwango bora kwa sasa Real Madrid.
Hata hivyo alinukuliwa akisema kuwa watahakikisha wanafanya kila njia kuhakikisha wanapata ushindi ili kuendeleza mbio zao za kuwania ubingwa.
"Tuna muda mrefu wa wiki nzima ya kufanya mazoezi na kujiandaa vyema kabla ya kuvaana na wapinzani wetu," Filipe alinukuliwa na tovuti ya klabu hiyo ya Atletico Madrid.
Beki huyo alisema kukabiliana na Real ni nafasi nzuri kwao ya kuthibitisha kuwa ni timu kubwa na matoeko ya jana hayawezi kuwavunja nguvu kwa sababu yanapaswa kusahauliwa na kuangali yaliyopo mbele yao.

No comments:

Post a Comment