STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 24, 2014

Ngumi zavumuka tena kanisa la Moravian

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/c/c1/AgnusDeiWindow.jpg
WIKI ya tatu mfululizo vurugu zimeendeleakatika kanisa la Moravian baada ya jana tena kuibuka kitimtim katika kanisa la Mwananyamala Msisiri A Kinondoni Dar Es Salaam. 
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alilidokeza MICHARAZO kuwa chanzo ilikuwa ni Maaskofu kutoka makao makuu ya kikanda ambao walifika na kutaka kuingia ndani ya Kanisa hilo na kuzuiwa na mmoja wa waumini.
Muumini huyo alidai kwamba Maaskofu hao wasiingie kwani mgogoro uliopo ndani ya kanisa hilo kwani utamalizwa na waumini wenyewe na kwamba kuwepo kwao kungechochea vurugu zaidi.
Wakati Maaskofu wakipinga amri hiyo, waumini ambao walikua ndani ikiwa ndio wanaanza ibada ya kwanza walisikia na ndipo wachache wakatoka nje, wengine wakishinikiza Maaskofu hao waingie huku wengine wakitaka waondoke.
Mabishano makali yaliyofuatiwa na ngumi yalizukabaina ya pande hizo mbili hadi maaskari ambao inaonekana walitonywa mapema hivyo kuwa karibu na eneo la tukio walipoingialia kati na kutuliza mtafaruku huo. 
Hata hivyo bado waumini walishinikiza kutoendelea na ibada hadi Maaskofu wa Kikanda waondoke eneo hilo na waumini kuamua kubaki nje badala ya kuendelea na ibada, wengine wakitimka kwa kuhofia vurugu zaidi.
Baadhi ya waumini waliokuwa wakiondoka walissikika wakisema kuwa heri wahamie makanisa mengine kwani hamkani si shwari tena kanisani hapo.
Inasemekana Maaskofu hao wa Kikanda walifika kanisani hapo ili kuamuru Baraza la Kanisa hilo kuvunjwa ili kupisha uchaguzi mwingine wa viongozi baada ya Baraza hilo kutuhumiwa kufuja pesa za kanisa kwa kutowasilisha mahesabu kwa waumini.
Udondozi zaidi umebaini kwamba kanisa hilo limekuwa na vurugu za chini chini ambazo inasemekana zimeanzia makao makuu ya Kanisa hilo, huku ikielezwa kwamba kumeibuka kambi mbili za uhasama, moja ikishinikiza viongozi waliopo sasa waondoke madarakani huku nyengine ikiunga mkono viongozi hao wabaki hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika.
Chimbachimba zaidi toka kwa shuhuda huyo zimebaini kwamba tatizo la msingi ni uongozi uliopo madarakani kutowasilisha mahesabu yaliyokaguliwa (Audited Account) ya Kanisa hilo lenye vitega uchumi vingi ikiwemo Chuo Kikuu cha Theophile Kisanji.
Mgogoro ambao ulifikishwa hadi Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo viongozi waliamuriwa kufanya mahesabu hayo na leo kuyawasilisha kwa waumini wao jambo ambalo halikufanyika hadi vurugu zilipoibuka tena.

No comments:

Post a Comment