STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 24, 2014

Hussein Bunu achekelea 'kuitungua' Simba Taifa


MSHAMBULIAJI wa JKT Ruvu, Hussein Bunu amesema amejisikia fahari mno kufanikiwa kuwatungua Simba na kupelekea kuipa kipigo timu hiyo kongwe akidai kuwa JKT walikuwa bora kuliko wapinzani wao.
JKT Ruvu iliizamisha Simba kwa mabao 3-2 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na Bunu alifunga bao la kuongoza dakika ya 13 tu ya mchezo kabla ya Emmanuel Switta kufunga mengine.
Akizungumza na MICHARAZO leo, Bunu alisema ingawa amekuwa akifunga mabao, katika mechi mbalimbali tangu aanze kucheza soka, lakini goli la juzi dhidi ya Simba limempata furaha kubwa kwa sababu limeibeba timu yao kuzoa pointi 3.
"Kwa kweli nimejisikia furaha sana kuwatungua Simba, bao langu nalitoa kwa familia yangu na hasa wanangu, naamini tulistahili ushindi kwani tulikuwa bora kuliko wapinzani wetu," alisema Bunu.
Bunu anayecheza pamoja na nduguye Abdallah Bunu katika timu hiyo alisema wachezaji wote wa JKT Ruvu walikuwa na lazima ya kushinda mechi hiyo baada ya kufanya vibaya mechi zao tatu zilizopita wakifungwa jumla ya mabao nane.
Walianza kwa kufungwa mabao 2-0 na Ruvu Shooting kisha kutoka suluhu na Oljoro kabla ya kuangamizwa 6-0 na Prisons.
Katika mechi hiyo ya jana mbali na Bunu mabao mengine yalioisaidia timu hiyo inayonolewa na kocha Fred Minziro yalifungwa na Emmanuel Switta aliyefunga mawili kabla ya Amissi Tambwe kuiopatia Simba mabao ya kufutia machozi.

No comments:

Post a Comment