STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, February 24, 2014

Mugabe asherehekea miaka 90 akipinga ushoga

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akisherehekea siku ya kuzaliwa kwake
 
RAIS mzee kuliko wote barani Afrika na aliyedumu madarakani kwa muda mrefu nchini Zimbabwe, Robert Mugabe jan Jumapili alisherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake mjini Harare. Katika hotuba iliyotolewa kwa zaidi ya saa nzima, Kiongozi  huyu mkongwe kabisa barani Afrika  alisema hataruhusu wapenzi wa jinsia moja nchini Zimbabwe. Alisema  hilo ndilo linalochangia kusambaa kwa virusi vya HIV na Ukimwi. Mugabe alinukuliwa na vyombo vya habari akielezea kuwa; “tumeumbwa kama wanaume na wanawake ili tuweze kuzaa watoto. Na hivyo ndivyo ilivyo.”
 Bw. Mugabe ambaye ametawala Zimbabwe tangu ilipopata uhuru wake mwaka wa 1980, alisema pia kuwa atapambana na ufisadi.
Matamshi yake yalifuatia kukamatwa kwa baadhi ya maafisa wa ngazi ya juu kutoka kwa shirika la ndege la kitaifa kutokana na  tuhuma za ufisadi uliohusisha dola milioni 10. Baada ya hotuba yake bwana Mugabe alikata keki kadhaa, mojawapo ikiwa na uzani wa kilo 90. Kisha wafuasi wake wakaanza kugawa zawadi ikiwemo mifugo 90 huku mfanyabiashara mmoja akimpa dola elfu 20 taslimu.
Sherehe hizo zaaminika kugharimu takriban dola milioni moja.Wanachama wa upinzani hawakuhudhuria sherehe hizo wakisema wanapinga kushindwa kwa bwana Mugabe kuokoa uchumi wa nchi unaozidi kuzorota. 
VOA

No comments:

Post a Comment