STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 16, 2013

Elias Maguli achekelea kuingia Stars na 'mguu' mzuri

https://fbcdn-sphotos-d-a.akamaihd.net/hphotos-ak-frc3/1461574_230784413749326_1852912229_n.jpg
MSHAMBULIAJI nyota wa Ruvu Shooting aliyeitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu B ya taifa, Elias Maguli, amesema anamshukuru Mungu kwa kuanza na mguu mzuri baada ya kufunga bao lililoizamisha Taifa Stars zilipoumana katikati ya wiki katika mechi ya kujipima nguvu.
Maguli ndiye mfungaji namba mbili kwa kupachika mabao mengi kwenye ligi kuu ya Bara iliyofika nusu msimu baada ya kupachika mabao tisa, moja nyuma ya Amisi Tambwe wa Simba na timu ya taifa ya Burundi.
Maguli alifunga bao hilo kwenye uwanja wa Karume kwa kumalizia pasi ya yosso wa Mtibwa Sugar, Juma Luizio ambao wote wamejumuishwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 32 wa Taifa Stars inayojiandaa kucheza Kombe la Chalenji.
Mchezaji huyo alisema anamshukuru Mungu kwa kumuongoza katika kila anachofanya na amefurahi kuingia na mguu mzuri Stars.
"Namshukuru Mungu kwa kila jambo (pamoja) na bahati hii niliyoingia nayo katika timu ya taifa ninayochezea kwa mara ya kwanza," alisema Maguli.
Maguli alisema atajibidiisha zaidi ili aendelee kudumu katika timu hiyo.
Stars iliyoanza kambi rasmi ya maandalizi ya Chalenji katikati ya wiki, itacheza pambano la kirafiki dhidi ya Harambee Stars ya Kenya Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa.
Baada ya pambano hilo wachezaji kutoka Zanzibar wataondoka katika timu hiyo kwenda kuungana na wenzao wa Zanzibar Heroes na waliobaki wataunda Kilimanjaro Stars itakayocheza Kombe la Chalenji kuanzia mwishoni mwa mwezi huu nchini Kenya.


No comments:

Post a Comment