STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, November 16, 2013

Hizi ndizo nasaha za Jonas Mkude kwa viongozi, makocha

Jonas Mkude

KIUNGO chipukizi wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amewataka viongozi wa soka na makocha kuthamini na kuwajali wachezaji ili wacheze kwa ufanisi uwanjani na kupata matokeo mazuri.
Mkude, ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, aliiambia MICHARAZO katika mahojiano maalum kuwa wachezaji vijana hukatishwa tamaa na baadhi ya mambo yanayofanywa na viongozi wao na makocha mara niyngine.
"Ili soka liweze kusonga mbele, ni lazima viongozi na makocha wabadilike na kuwajali na kuwathamini wachezaji na kuwasaidia pale wanapoonekana kukosea kuliko kuwakatisha tamaa," alisema Mkude bila kufafanua.
Aidha Mkude alisema upo ulazima wa kuwekeza katika soka la vijana kwa ajili ya kutafuta mafanikio kimataifa.
"Soka la vijana ndiyo ukombozi wa kandanda la Tanzania," alisema Mkude na kueleza zaidi kuwa "hata mataifa ya nje yamefika yalipo kwa kuwekeza katika soka la vijana kitu ambacho nasi tunapaswa kuiga kufikia mafanikio ya kweli," alisema.
Mkude aliyesajiliwa na Simba mwaka 2010 akitokea Mwanza United alisema anaamini Tanzania itaacha kuwa msindikizaji katika anga ya kimataifa kama nguvu kubwa zitawekwa kwa vijana na kupewa maandalizi mazuri.

No comments:

Post a Comment