STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, February 20, 2014

ALLY CHOKI AWAPA VIDONGE WAPINZANI WAKE

* Awaambia washindane jukwaani siyo maneno ya mitaani
* Asema Extra Bongo wapo kikazi zaidi kuliko 'kutafutana'
Ally Choki (kushoto) akizungumza na wanahabari, huku Juma Kasesa Msemaji wa bendi akiwa makini kumsikiliza
Jenerali Banzastone (kushoto) akifafanua jambo huku dansa kiongozi wa Extra Bongo akisikiliza kwa makini wakati wa mkutano wa wana Extra Bongo na wanahabari, kwenye ukumbi wa Heikein Mbagala Kuu.
Wanahabari wakiwa makini katika mkutano huo wa leo
Madansa wa kiume wa Extra Bongo wakionyesha manjonjo yao kwa wanahabari

Ally Choki mwenye mic, akiwachezesha madansa wa kike katika mkutano wa wanahabari juu ya kambi ya maandalizi ya uzinduzi wao utakaofanyika Jumamosi pale Dar Live

MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo 'Wana Kimbembe', Ally Choki 'Mzee wa Farasi' a.k.a Kamarade amewashukia wapinzani wake kimuziki kwa kuwaambia yeye hataki kushindana kwa maneno ya mitaani bali anataka wapimane ubavu jukwaani kupitia kazi zao za muziki.
Choki alitoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na wanahabari kwa kudai kuwa kumekuwa na mashambulizi ya maneno toka kwa wapinzani wake kimuziki na kuiandama bendi yao, lakini alisema yeye hana muda wa kuwajibu kwa sababu yeye kazi ya ni muziki.
Mtunzi na muimbaji huyo aliyewahi kutamba na bendi kadhaa zikiwamo Extra Kimwa, The Bantu Group, TOT-Plus, African Stars 'Twanga Pepeta' na Mchinga Generation 'Timbatimba', alisema washindani wake nawataka wakutane kwenye jukwaa la muziki na siyo blabla naa maneno yasiyo na tija.
"Wapo wanaotuandama na kutushambulia kwa maneno na kuiandama bendi yetu ila sisi hatuna muda wa kujibishana nao, sisi tunataka tushindane na kupimana jukwaani siyo maneno ya mitaani," alisema Choki.
Aliongeza kuwa kutokana na kwamba yeye huwa habahatishi katika zinduzi za bendi au albamu mashabiki watarajie makubwa siku ya Jumamosi ambapo Extra Bongo watazindua albamu ya 'Mtenda Akitendewa'.
"Mashabiki waje waone mtumishi wao nitawafanyia nini, ila tumejipanga kuwapa burudani ya uhakika ambayo hawajawahi kuipata kwa siku za karibuni, kwani kutakuwa na manjonjo mengi kama kawaida yangu ila siwezi kuwaambia nitaingiaje ukumbini siku hiyo, ila kuna bonge la Surprise nimeandaa," alisema Choki.
Extra Bongo watazindua albamu hiyo ambayo ni ya pili kwa bendi yao baada ya awali kutamba na 'Mjini Mipango', kwenye ukumbi wa Dar Live a.k.a Uwanja wa Taifa wa Burudani ambapo mashabiki watapata audio na video siku hiyo ya uzinduzi ili kukata kiu yao ya burudani.

No comments:

Post a Comment