STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 29, 2012

Shabani Kilumbelumbe kuzichapa na Mnamibia

Bondia chipukizi Mtanzania, Shabani Kilumbelumbe Novemba 13, anatarajiwa kupanda ulingoni jijini Windhoek-Namibia kuzipiga na Emmanuel Naidjala 'The Prince' wa Namibia katika pambano la raundi 12 kugombea ubingwa wa WBO-AFRICA .
Pambano hilo ni la uzito wa bantam-kgs 53.5 na litafanyika katika ukumbi wa Windhoek Country Club Resort.

Promota wa pambano hili ni Nestory Thobias wa Nestory Sunshine Boxing ya Namibia.

TPBO tayari imeshapata barua ya mwaliko kutoka Chama cha Ngumi na Mieleka cha Namibia na mktaba wa bondia pia umeletwa kwa TPBOkupitia wakala wa pambano hili  Julius Odhiambo wa Kenya .

Tayari Meneja wa Kilumbelumbe Mwalimu Hatibu ameshapewa taarifa kuhusu bondia wake kukabiliwa na pambano hili chini namibia.

TPBO imemtaka meneja huyo kumuandaa bondia hiyo kwa ajili ya pambano hilo ili aweze kuipeperusha vema bendera ya taifa.



No comments:

Post a Comment