STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 13, 2013

BARCELONA YAFANYA MAANGAMIZI ULAYA

 

'Mchawi Mweupe' Lionel Messi akishangilia moja ya mabao yake mawili usiku wa jana.

NI Maangamizi! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya vinara wa Ligi Kuu ya Hispania, Barcelona usiku wa kuamkia leo kuifumua bila huruma AC Milan ya Italia na kutinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya bila kutarajiwa.
Mabao mawili ya 'Mchawi Mweupe' Lionel Messi na mengi ya David Villa na Jordi Alba, imeifanya Barca kutinga hatua hiyo kwa kuitupa nje AC Milan kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya mechi ya awali kuchezea kipigo cha mabao 2-0 ugenini.
Messi aliendelea kuimarisha rekodi yake ya mabao katika michuano ya msimu huu kwa kufunga bao la kwanza dakika ya tano akimalizia kazi nzuri ya Xavi, kabla ya kuiongeza jingine dakika tano kabla ya mapumziko kwa shuti kali kwa pasi murua ya Iniesta na kuifanya Barca iende mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili, AC Milan wakiingia wakitafuta mbinu za kuweza kudhibiti mashambulizi ya wenyeji wao, lakini wakajikuta wakitungulia bao la tatu kupitia kwa Villa aliyemegewa pande tamu na Xavi na kufunga dakika ya 55.
Bao lililoikata maini AC Milan ambayo kupitia nyota wake Robinho, Kevin Prince Boateng, Sule Muntari walijaribu kufurukuta bila mafanikio, lilitumbukizwa kimiani na Alba dakika za nyongeza pambano hilo na kuifanya Barca kuweka historia kwa timu iliyonyukwa mabao 2-0 katika mechi ya kwanza kusonga mbele katika michuano hiyo ya Ulaya.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo iliyochezwa usiku wa jana, wenyeji Schalke 04 walijikuta wakinyukwa nyumbani na wageni wao Galatasaray kwa mabao 3-2 na kung'oka kwenye michuano hiyo.

Kikosi cha Galatasaray kilichokuwa na Didier Drogba kilishtukizwa kwa kufungwa bao la dakika ya 18 kupitia Roman Neustadter kabla ya Hamit Altintop kusawazisha katika dakika ya 37 na Burak Yilmaz kuiongezea wageni bao la pili katika dakika ya 42.
Michael Bastos aliipatia Schalke bao la kusawazisha katika kipindi cha pili kwenye dakika ya 63 na wengi kuamini mechi hiyo ingeisha kwa sare hivyo ambapo jumla ya matokeo yalikuwa yakisomeka 3-3 kutokana na sare ya baoa 1-1 waliyopata timu hizo katika mechi ya ya kwanza, Galatasaray walipata bao la tatu.
Bao hilo lililwekwa kiminia kwenye dakika za nyongeza za pambano hilo kupitia kwa Umut Bulut na kuivusha timu yake hadi robo fainali ya michuano hiyo mkubwa kwa ngazi za klabu barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment