STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 12, 2013

Kim Poulsen kuanika silaha za kuivaa Morocco

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen
Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen kesho anatarajia kuanika kikosi cha timu yake kitakachovaana na Morroco katika pambano la kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014.
Kim atazungumza na wanahabari kesho majira ya saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 24 mwaka huu katika mechi ya kundi C ikiwa sambamba na Ivory Coast na Gambia.
Mpaka sasa Stars inashika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi lake ikiwa na pointi 3 moja nyuma ya ilizonazo Ivory Coast wanaoongoza msimamo na ambao wikiendi hii nao watashuka dimbani kucheza na Gambia.
Stars inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kuweka hai matumaini yta kufuzu fainali hizo za Kombe la Dunia ambazo zitafanyika mwakani nchini Brazili.
Msimamo wa kundi walilo Stars ni kama ifuatavyo:

                                   P  W  D  L   F  A  GD PTS
1. Ivory Coast             2   1   1   0   4   2    2   4
2. Tanzania                  2   1   0   1   2   3   -1   3
3. Morocco                 2   0   2   0   3   3    0   2
4. Gambia                    2   0   1   1   2   3  -1   1

No comments:

Post a Comment