STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 12, 2013

Yanga yaipigia hesabu Ruvu Shooting

 
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inaendelea kujifua kwa mazoezi makali kwa ajili ya pambano lake lijalo dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting litakalochezwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar.
Yanga inayoongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 45 na mabao 36 ya kufunga na mabao 12 ya kufunga, inahitaji ushindi katika mechi hiyo ijayo ili kuzidi kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa amnbao unashikiliwa kwa sasa na Siumba iliyopo nafasi ya tatu ikiwa  na pointi 34, tatu nyuma ya Azam.
Baada ya kupata ushindi wa nne mfululizo kwa kuilaza Toto Africans, vijana hao wa Ernest Brandts wapo katika mazoezi makali katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ikiwa maandilizi ya mechi hiyo ya Jumamosi.
Katika mazoezi ya jana kikosi hicho kiliwakosa nyota wake Kelvin Yondani na Said Bahanuzi ambao ni majeruhi.
Yondani anasumbulia na maumivu ya dole gumba aliloumia kwenye mchezo dhidi ya Toto Africans na Bahanuzi alishtua msuli wa kisigino na kwa mujibu wa daktari wa timu Dk Nassoro Matuzya wachezaji hao wanaendelea vizuri na huenda leo wakajumuika na wenzao kuendelea na mazoezi.
Pia Dk Matuzya alisema mchezaji Ladislaus Mbogo anatazamiwa kufanyiwa upasuaji wa uvimbe (shavuni) leo.
Mbogo atafanyiwa upasuaji huyo baada ya klabu ya Yanga kuridhia kufuatia  uchunguzi uliofanywa na madaktari juu ya uvimbe huo na kwa maana hiyo mchezaji huyo atakosa mechi kadhaa za timu yake.

No comments:

Post a Comment