STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 27, 2014

Man City vs Chelsea, Arsenal vs Liverpool FA CupDROO ya Raundi ya 5 ya FA CUP imefanyika leo ambapo bahati imezikutanisha vigogo vilivyopo kwenye Top 5 ya Ligi ya England, ambapo Manchester City itaavana na Chelsea na Arsenal itakutana na  Liverpool.
Mechi zingine zitakazohusisha timu za Ligi Kuu ya England ni kati ya Sunderland v Southampton na Everton v Swansea.
Mechi hizi zitachezwa wikiendi ya Februari 15 na 16 na Washindi kutinga Robo Fainali.
Droo hiyo ilifanyika huko Wembley Stadium Jijini London na kuendeshwa na Andros Townsend, Mchezaji Chipukizi wa Tottenham, pamoja na Baba yake Mzazi, Troy, ambae ni Mwanaharakati maarufu kwenye Soka.
RATIBA KAMILI:
Manchester City v Chelsea
Sheffield United AU Fulham v Nottingham Forest AUr Preston NE
Arsenal v Liverpool
Brighton v Hull
Cardiff City v Wigan
Sheffield Wednesday v Charlton
Sunderland v Southampton
Everton v Swansea

No comments:

Post a Comment