STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 17, 2014

Azam watangulia Robo Fainali Kagame


MABINGWA wa soka nchini Azam wamefanikiwa kutinga hatua ya Robo fainali ya michuano ya Kagame baada ya kuibamiza Adama ya Ethiopia kwa mabao 4-1 katika mechi iliyocheza mjini Kigali, Rwanda.
Mechi hiyo iliyokuwa ya kukamilisha ratiba kwa Azam katika hatua ya makundi lilichezwa kwenye uwanja wa Nyamirambo na  maboa ya washindi yaliwekwa kimiani na nahodha, John Bocco 'Adebayor', Mcha Khamis 'Vialli', Didier Kavumbagu na Kipre Tchetche.
Ushindi huo umeifanya Azam kuongoza kundi lake kwa kuwa na pointi 8 baada ya sare mbili na ushindi wa mechi mbili na sasa itashuka dimbani Jumatano kuumana na El Merreikh ya Sudan.
Azam waliingia kwenye michuano hiyo kama zali baada ya waliokuwa wawakilishi wa Tanzania, Yanga kuenguliwa kwa kitendo cha kutaka kupelekea kikosi cha pili katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za klabu kwa timu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Hii ni mara ya pili kwa Azma kuicheza michuano hiyo, mwaka 2012 iliishiriki wakati Tanzania ikiwa wenyeji na ilifanikiwa kufika fainali na kufungwa mabao 2-0 na Yanga iliyokuwa imetwaa kwa mara ya pili mfululizo.

No comments:

Post a Comment