STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 17, 2014

Maafa! Jiwe laporomoka na kuua wanne Mwanza

http://radio-tanzania.de/wp-content/uploads/Bismarck-Rock.jpg
WATU wanne wa familia mbili tofauti wa  barabara ya Nyerere ‘A’ katika eneo la Mabatini wilayani  Nyamagana jijini Mwanza, wamefariki baada ya kuporomokewa na  jiwe kubwa lililoviringika kutoka mlimani kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi.
Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi waliofariki ni pamoja na Sayi Otieno na mkewe Quenter Kweko walifariki papo hapo baada ya kukandamizwa na jiwe kubwa lilivunja nyumba waliyokuwa wakiishi eneo hilo, huku mtoto wao mwenye miaka 4 akinusurika kifo.
Baada ya jiwe hilo kuleta madhara katika nyumba hiyo, pia likalisukuma jiwe jingine ambalo liliporomoka na kuipiga nyumba ya Joseph William na kuwaua watoto wake wawili papo hapo waliotajwa Keflin Masalu (14) na Emaueli William (12) anayesoma darasa la tano huku Jophrey Joseph (14) wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mbugani akinusurika.

Polisi na uongozi wa serikali ya Mwanza imewataka wakazi waliojenga kwenye milima ya mawe na kuhatarisha maisha yao kuhama katika maeneo hayo kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha ili kuepuka maafa zaidi.

No comments:

Post a Comment