KOCHA
wa timu ya taifa ya Nigeria, Stephen Keshi bado yuko katika mshangao
kufuatia kipigo walichopata kutoka kwa Sudan katika mchezo wa kufuzu
michuano ya Mataifa ya Afrika.
Super Eagles
walishindwa kucheza kwa kiwango chao cha juu na kujikuta wakichapwa bao
1-0 katika Uwanja wa Manispaa jijini Khartoum katika mechi za kuwania Fainali za Kombe la Afrika mwakani.
Keshi amesema kikosi
chake kingeweza kuibuka na ushindi katika mchezo huo kama nafasi
walizotengeneza zingetumika ipasavyo lakini haraka aliwaomba radhi
mashabiki wa Nigeria kwa kupoteza mchezo huo.
Kocha huyo amesema inabidi
aombe radhi kwani mashabiki wa Nigeria walikuwa na imani kubwa na timu
yao kuibuka na ushindi.
Mbali na Keshi lakini pia golikipa na nahodha wa
Super Eagles Vincent Enyeama naye aliwaomba radhi mashabiki kwa kipigo
hicho na niaba ya wachezaji wenzake na kuahidi kufanya vyema katika
michezo yao inayofuata.
No comments:
Post a Comment