SHIRIKISHO
la Soka Afrika, CAF, limeichomolea Morocco wenyeji wa Fainali za Afrika za mwakani, ambao waliomba kuahirishwa kwa michuano hiyo kwa hofu ya ugonjwa wa EBOLA.
CAF wamesisitiza kuwa fainali hizo za mataifa ya Afrika
2015 itaendelea kama ilivyopanga licha ya hofu ya wenyeji dhidi ya ugonjwa huo hatari.
Morocco waliomba shindano hilo liahirishwa kufuatia mripuko wa
ugonjwa huo ambao umeua watu zaidi ya 4,000 baada ya maafisa wa afya
nchini humo kuonya kuendelea kwa fainali hizo kwa madai yanaweza kuendeleza uambukizaji zaidi.
Mshauri wa Waziri wa Michezo wa Morocco, Mohammed Ouzzine, alieleza
taifa hilo la magharibi mwa bara hilo lina wasiwasi kuandaa shindano
hilo linalochukua wiki tatu.
“Matakwa ya Morocco na wakaazi wake pamoja na wale wa bara Afrika
yanadunisha linguine lolote. Morocco wamewasilisha ombi hilo kufuatia
ushauri muhimu kutoka maafisa wa afya.
“Hatuwezi hatarisha maisha ya watu kwa kuendelea kuandaa shindano
hili kwani msingi wa tahadhari unafaa kufuatwa,” mshauri Hamid Faridi
aliambia stesheni ya redio, Atlantic Jumamosi.
Kwa majibu, Caf walitoa taarifa wakitofautiana na wenyeji hao huku
Afrika Kusini wakilengwa kama waandalizi wa dharura ikiwa Morocco
watajiondoa.
“Caf wanadhibitisha hakuna badiliko kwenye ratiba ya shindano hili.
Tungependa kukumbusha kwamba tangu dimba la kwanza la 1975, shindano
hili halijawahi chelewa au kuhairishwa,” taarifa ya utawala huo wa
kandanda ilisema.
Mataifa ya Afrika magharibi, Guinea, Liberia na Sierra Leone
yameadhirika zaidi na mkurupuko wa sasa wa Ebola. Guinea na Sierra Leone
bado wanawania tiketi za Morocco 2015.
Afrika Kusini waliokoa jahazi la shindano hilo 1996 na mwaka jana.
No comments:
Post a Comment