KLABU ya Arsenal imezidi kupata pigo baada ya nyota wake kadhaa kupata majeraha, kufuatia kuumia kwa beki Laurent Koscielny aliyelazimika kujiondoa
kwenye mazoezi ya timu yake ya kitaifa ya Ufaransa.
Beki huyo wa kati amejitoa Les Blues kutokana na maumivu ya ukano
wa kisigino.
Meneja
Arsene Wenger amepigwa na pigo moja baada ya lingine ikiwa ni mechi saba tu
ndani ya msimu mpya huku ambapo sasa Koscielny anajiunga na nyota wenzake
Danny Welbeck, Mathieu Debuchy, Mikel Arteta, Olivier Giroud, David Ospina, Aaron Ramsey na
Yaya Sanogo kwenye zahanati.
Siku mbili
baada ya Ujerumani kutangaza kiungo nyota Mesut Ozil atalazimika kutocheza kati
ya wiki 10 na 12, Wenger ameongezewa tumbo joto na habari kuwa beki Koscielny
amejiondoa kutoka mechi za Ufaransa dhidi ya Ureno na Armenia kwenye msururu wa
kufuzu Kombe la Euro la 2016, huku Danny Welbeck naye akiiumia wakati England ikishinda 1-0.
Shirikisho
la Ufaransa limeandika kwenye anwani yao ya mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa
Koscielny anauguza uvimbe wa ukano wake wa kisigino.
No comments:
Post a Comment