STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 16, 2013

CCM, CHADEMA VITA TUPU IRINGA, MORO

MWENYEKITI wa Baraza la Wazee wilayani Kilolo, Lunyiliko Nyaulingo amelazwa katika Hospitali ya mkoa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mgololo amelazwa Hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu wanaodaiwa ni wanachama wa CCM katika kampeni za mwisho za kuwania nafasi ya udiwani.

Sambamba na hiyo Katibu wa CCM kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo, Wilhad Ngogo (40) na Yohana Mchafu anayedaiwa kuwa ni mwanachama wa CCM wanashikiliwa na Polisi kwa kuhusika na matukio hayo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema watu hao walikamatwa jana kufuatia 
vurugu zilizojitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya mwisho katika wilaya hizo mbili.

Alisema kufuatia mzozo huo wanachama wa CHADEMA walizuia barabara ya Iringa-Mbeya kwa kuweka magogo ili kuzuia magari kupita na kuwa Polisi wanamtafuta Rabart Sam maarufu kwa jina la Kideri kwa kuongoza vurugu hizo.

Kamanda Mungi alisema wanafanya uchunguzi wa kina juu ya matukio hayo na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wote wa vyama vya siasa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuepusha vurugu ambazo zinaweza kutokea.

Leo Uchaguzi wa udiwani katika kata ya Ng’ang’ange wilayani Kilolo na Mbalamaziwa wilayani Mufindi ulifanyika ambapo Zuberi Nyomolelo (CCM) na Ezekiel Mlyuka (CHADEME) walipambana kwa kata ya Mbalamaziwa na kwa upande wa Ng’ang’ange Kilolo Nafred Chahe (CHADEMA) na Namgalesi Msuva (CCM) walipambana.

Tukio hilo limejiri wakati huko Morogoro nako inaelezwa wanaodaiwa vijana walinzi wa CCM kuwakata mapanga viongozi wa CHADEMA, huku watanzania wakiendelea kuomboleza tukio la mlipuko wa bomu jijini Arusha lililopoteza uhai wa watu wawili na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Katibu  Mwenezi wa tawi la Minepa, Jimbo la Ulanga Magharibi, Severin Matanila aliyekaa aliyejeruhiwa katika tukio la Morogoro, huku viongozi wenzake, Mwenyekiti wa Jimbo, Kibam Ally Mohammed na Katibu wake, Lucas Lihambalimo (aliyeipa kamera mgongo) wakiwa pembeni yake 
via Mjengwa

No comments:

Post a Comment