STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 16, 2013

Ntiro, Nyagawa waibeba Golden Bush Veterani wakiilaza Mburahati Veterani 3-2

Onesmo Waziri 'Ticotico' akimiliki mpira langoni mwa Mburahati, huku Salum Swedi (11) akiwa tayari kutoa msaada.

Hekaheka langoni mwa Mburahati baada ya Machota (2) kukaribia kufunga bao

Peter Kalumbeta (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka Shija Katina wa Golden Bush

Mohammed wa Mburahati akichuana na Shomari

Nico Nyagawa 'akikusanya kijiji' kwa kuwatoka wachezaji wa Mburahati Veterani
Faraji wa Golden Bush (kulia) akikokota mpira huku akifuatwa na beki wa Mburahati huku Abuu Ntiro akiwa tayari kumsaidia wakati timu zao zilipoumana asubuhi ya leo.
Wachezaji wa Golden Bush Veterani wakati wa mapumziko
 
Kudra Omar wakati wa mapumziko
Nico Nyagawa akitafakari wakati wa mapumziko
Onesmo Waziri 'Ticotico' akichuana na wachezaji wa Mburahati huku Nahodha wake Yahya Issa akiwa makini kumsaidia

Yahya Issa akiambaa na mpira mbele ya mchezaji wa Mburahati
Salum Swedi (11) akiambaa na mpira huku akichungwa na beki wa Mburahati Veterani

Mshambuliaji nyota wa zamani Atufugwegwe Mwakalukwa (kushoto) akiwa na wachezaji wenzake wa Mburahati nje ya uwanja
Benchi la timu ya Mburahati Veterani wakiwa hawaamini kama Golden Bush wamewashika leo kwenye uwanja wa Chuo Kikuu

Mchezaji wa Mburahati akiambaa na mpira huku mwenzake akiwa makini kumsaidia

Peter Kalumbeta wa Mburahati (kulia) akimtoka beki wa Golden Bush
WAKATI vijana wao jana kulala mabao 2-0 mbele ya Simba, timu ya Golden Bush Veterani leo asubuhi wamejifariji baada ya kuinyuka Mburahati Veterani kwa magoli 3-2 katika mchezo wa kirafiki.
Vijana wa Golden Bush walilala kwa Simba katika pambano lililochezwa jana jioni kwenye uwanja wa Kinesi, lakini wazee wao walifanya kweli viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Golden Bush Veterani ambayo wiki kadhaa ilikuwa 'baba huruma' kwa kuchezea vipigo kwa wapinzani wao, walianza kuandika bao katika kipindi cha kwanza kupitia Abuu Ntiro.
Licha ya Golden Bush iliyosheheni nyota waliowahi  kutamba nchini kama ivo Mapunda, Salum Swedi 'Kussi', Nico Nyagawa, Yahya Issa, Kudra Omar, Wisdom Ndlhovu, Steven Marashi na wengine kusakama lango la Mburahati matokeo yalibaki bao 1-0 hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ya wachezaji na kwa kiasi fulani ilibadili kasi na Mburahati ilifanikiwa kusawazisha bao kupitia shuti kali lililopigwa na Peter Kalumbeta.
Hata  bao hilo lilidumu kwa dakika moja tu kwani Nico Nyagawa alifunga bao la pili la Golden Bush akimalizia kazi nzuri ya Shoamri aliyepanda mbele.
Winga msumbufu wa Mburahati Ally 'Neymar' alifunga bao la kusawazisha kwa timu yake baada ya kuwatoka mabeki wa Golden Bush na kupiga shuti lililomshinda kipa Steven Marashi.
Dakika za lala salama baada ya kulilia kuingizwa dimbani, Machota alionyesha hakulilia bure kucheza mechi hiyo kwani aliiandikia Golden Bush bao la tatu na la ushindi kwa kichwa akimalizia krosi safi ya De Natale.
Mbuharati alikaribia kupata bao la kusawazisha kama sio uzembe uliofanywa na winga wao wa kulia, Karume kushindwa kutumbukiza wavuni mpira akiwa yeye la lango kufuatia kroshi ya 'Neymar'.
Mpaka filimbi ya mwamuzi Madaraka Seleman 'Mzee wa Kiminyio' ikilia kuashiria mwisho wa pambano hilo Golden Bush waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-2 mbele ya wapinzani wao, Mburahati iliyowakosa baadhi ya nyota wao kama Abdul na Juma Chilumba na Atufugwegwe Mwakalukwa katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment