STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 28, 2013

Serikali yayafungia magazeti za MWANANCHI na MTANZANIA, kisa...

Moja ya magazeti yaliyofungiwa na serikali
 HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni Michezo na Vijana, imeyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kutokana na kile kilichoelezwa kukaidi maonyo ya kuacha kuandika habari za kichochezi.
Taarifa hiyo imesema kuwa Mwananchi limefungiwa kwa muda wa wiki mbili na lile la Mtanzania limefungiwa kwa siku 90 sawa na miezi mitatu.
Kufungiwa kwa magazeti hayo ni muendelezo wa adhabu ambazo serikali imekuwa ikivichukulia vyombo vya habari kutokana taarifa zao wanazochapisha au kutangaza zinazokinzana nayo kama ilivyowahi kulikuta gazeti la Mwanahalisi ambalo mpaka sasa bado lipo kifungoni.
Wengine waliowahi kukumbana na rungu la serikali ni gazeti la Majira na vituo vya redio Imani Fm na nyingine ya kidini ya mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment