STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 28, 2013

Yanga yazinduka, Kagera yaipumulia Simba,


HATIMAYE mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ikimchezesha kwa mara ya kwanza kiungo mshambuliaji wake nyota, Mrisho Ngassa, imezinduka leo kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuidonoa Ruvu Shooting ya Pwani kwa bao 1-0.
Ushindi huo wa pili kwa mabingwa hao watetezi kwa msimu huu, umewafanya wafikishe pointi 9 na kuchupa hadi nafasi ya nne toka nafasi ya tisa iliyokuwa ikikamata ikiwa inalingana na JKT Ruvu ambayo kesho itashuka dimbani kupepetana na Simba, Azam na Ruvu Shooting wakitofautiana uwaiano wa mabao yao tu.
Yanga ambayo imetoka kuchezea kipigo cha mabao 3-2 toka kwa Azam na kuambulia sare tatu mfululizo,leo ilionyesha dhamira ya kuibuka na ushindi kwa kuishambulia kama nyuki wapinzani wao ambapo hata hivyo umahiri wa kipa Abdul Seif uliwakatisha tamaa na kufanya hadi mapumziko mambo yawe 0-0.
Bao lililowapa faraja Yanga jioni yua leo lilifungwa dakika ya 62 na Hamis Kiiza 'Diego' kwa 'tiktak' akimaliza pasi ndefu iliyotumwa na Ngassa aliyepokea pasi murua ya Mbuyi Twitte.
Hata hivyo ni mpaka alipoingia Athuman Idd Chuji katika kipindi hicho cha pili na kubadilisha mchezo ndiyo Yanga ilipoonyesha uhai, baada ya dakika 45 za awali kubanwa vilivyo na Ruvu japo ilishambulia mara kadhaa na kukatishwa tamaa na kipa aliyekuwa Abdul Seif aliyekuwa akidaka michomo na kufanya mbwembwe uwanjani.
Katika michezo mingine ya leo Kagera Sugar imefanikiwa kuitungua Rhino Rangers nyumbani kwao Tabora kwa bao 1-0 na kukwea hadi nafasi ya pili ikilingana pointi na Simba zote zikiwa na 11 zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Bao wa washindi hao lilifungwa na Themi Felix, huku ikishuhudiwa wenyeji wakicheza pungufu baada ya Nudrin Bakar kulimwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Kagera.
Nayo Coastal Union ilishindwa kulinda bao lao lililotupia na Haruna Moshi 'Boban' na kulazimishwa sare ya bao 1-1 ugenini na wenyeji wao Mbeya City. hata hivyo Boban alilimwa kadi nyekundu katika mchezo huo baada ya kumkutana mwamuzi wa pembeni na kuifanya Coastal kumaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya mchezaji wake mwingine kutolewa na mchezaji wa Mbeya City walipotaka kupigana uwanjani.
Katika mchezo mwingine uliyechezwa uwanja wa Mkwakwani Tanga, wenyeji Mgambo JKT walishindwa kutambiana na Oljoro JKT ya Arusha baada ya kutoka suluhu ya kutiofungana.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mechi za leo
                                   P  W  D  L   F   A  GD  PTS
1.  Simba                     5   3   2   0  13  4    9   11
2.  Kagera Sugar          6   3  2   1   7   3    4   11
3. Coastal Union          6   2  4   0   6   3   3   10
4. Yanga                      6   2  3   1  11  7   4   9
5. JKT Ruvu                5   3   0   2   6   2   4    9
6.  Azam                     5    2  3   0   8   5   3    9
7.  Ruvu Shooting        6   3  0   3   6   4   3    9
8.  Mbeya City           6   1  5   0   6   5   1    8
9.  Rhino Rangers       7   1  4   2   7  8    -1   7
10.Mtibwa Sugar        5   1  3   1   3  4   -1   6
11.Oljoro                    6   1   2   3   3   6  -3   5
12.Mgambo               6   1   2   3   2  10 -8   5
13.Prisons                  5   0   3   2   2    8  -6   3
14.Ashanti                  6   0   1   5   2  13 -11  1

No comments:

Post a Comment